Перейти к содержимому

JINSI YA KUJENGA MFUKO WA DHARURA | Emergency Fund 💰🔥

Coach Rahabu

0:00 / 0:00

JINSI YA KUJENGA MFUKO WA DHARURA | Emergency Fund 💰🔥

89 просмотров · 9 дн. назад
Coach Rahabu
34 подписчика
89 просмотров · 9 дн. назад
Kama kipato chako kingesimama leo, unaweza kuendelea kuishi bila kukopa? 🤔💰 Dharura inaweza kutokea wakati wowote kama kupoteza kazi, biashara kuyumba, gharama kubwa isiyotarajiwa ya maisha au kipindi ambacho kipato hakitoshi. Tatizo siyo kwamba hatujui mambo haya yanaweza kutokea, tunajua kabisa lakini; tatizo ni kwamba wengi wetu hatujiandai kabla hayajatokea. Kwenye episode hii ya Living With Coach Rahabu, tunazungumzia Mfuko wa Dharura (Emergency Fund) ni nini, kwa nini ni muhimu, madhara ya kutokuwa nao na, muhimu zaidi, jinsi ya kuujenga hatua kwa hatua kulingana na kipato na gharama zako za maisha ya kila siku. Tutafanya pia calculation rahisi za Emergency Fund ili uweze kujua unahitaji kiasi gani, uanze na kiasi gani na unaweza kufikia target yako kwa muda gani. Hata kama kipato chako ni kidogo au kinabadilika, usione kama huwezi kuanza. Emergency Fund inaanza na kiasi kidogo unachoweza kuweka kwa consistency. Lengo siyo kuwa na pesa nyingi tu. Lengo ni kuwa na financial security, nafasi ya kupumua na machaguo wakati maisha yanapobadilika. Kwenye video hii utajifunza: Mfuko wa Dharura ni nini na unatumikaje? Hasara za kutokuwa na Emergency Fund Faida za kuwa na Mfuko wa Dharura Jinsi ya kuhesabu kiasi unachohitaji Mfano wa calculation kwa kipato tofauti Jinsi ya kuanza ku-save Emergency Fund Wapi pa kuweka pesa ya dharura Nini cha kufanya ukilazimika kuitumia Jinsi ya kuijenga tena baada ya emergency Usisubiri dharura itokee ndiyo uanze kutapatapa na kujutia - hii inaweza kuepukika kwa asilimia kubwa. Anza na kile ulicho nacho. Anza kidogo. Anza leo. 💬 SWALI LA LEO: Kama kipato chako kingesimama leo, ungeweza kuishi kwa miezi mingapi bila kukopa....? Andika jibu lako kwenye comments. Kama video hii imekusaidia, LIKE, SHARE na SUBSCRIBE kwenye Living With Coach Rahabu kwa mazungumzo zaidi kuhusu maisha, fedha, personal growth, investment na kujenga future yenye uhuru na machaguo. #EmergencyFund #MfukoWaDharura #Saving #PersonalFinance #FinancialFreedom #MoneyManagement #FinancialLiteracy #SavingMoney #Uwekezaji #Fedha #Tanzania #SwahiliYouTube #LivingWithCoachRahabu