KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING / 08 OCTOBER 2026
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
0:00 / 0:00
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING / 08 OCTOBER 2026
3 830 просмотров · Трансляция закончилась 2 ч назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
65,3 тыс. подписчиков
3 830 просмотров · Трансляция закончилась 2 ч назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING / 08 OCTOBER 2026
SOMO : VISHINDE VIKWAZO VINAVYOKUSONGA ILI UWE NA MATOKEO
Marko 5 : 22 - 34
22 Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,
23 akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.
24 Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa.
25 Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili,
26 na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya
27 aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.
29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.
30 Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?
31 Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa?
32 Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo.
33 Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote.
34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
NAMNA YA KUJIPENYEZA NA KUWA NA MGUSO WENYE MATOKEO BILA KUONDOA VIKWAZO
1. Jitofautishe na wengine kimtazamo, kifikra na kiutendaji.
Wakati mwingine tunashindwa kuwa na matokeo si kwasababu ya msongamano au vikwazo ila ni kwasababu tumeshindwa kujipenyeza, na tunajaribu kufanya kama wengine wanavyo Fanya bila kujua udhaifu tulionao
Mfano
Daudi hakutumia siraha wala mfumo wa kijeshi kumshida Goliath alitukia kombeo na jiwe
1 Samweli 17 : 38 - 40
38 Ndipo Sauli akamvika Daudi mavazi yake ya vita, akamtia chapeo cha shaba kichwani, akamvika dirii.
39 Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu. Basi Daudi akavivua.
40 Akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti.
2. Jipenyeze Kwa kufanya mambo tofauti na kawaida ilivyozoeleka.
Marko 14 : 3 - 9
3 Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.
4 Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii?
5 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung'unikia sana yule mwanamke.
6 Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema;
7 maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.
8 Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko.
9 Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
3. Chukuwa hatua juu ya unachokiwaza na unachokiamini.
Marko 5 : 28
4. Usipoteze nguvu nyingi kuondoa kikwazo, wakati unaweza kutumia nguvu kidogo kwa kujipenyeza na kupata matokeo bila kuondoa kikwazo na katikati ya msongamano ukapata matokeo.
Mfano
Paulo hakusubiri gereza liondoke ndipo huduma yake iendelee; alitumia mazingira ya gereza kuzaa matokeo ambayo yangepita hata nje ya gereza.
Wafilipi 1 : 12 - 13
5. Sio kila kiwazo ni cha kuondoa kuna vingine vipo na vimewekwa ili kuyapa thamani matokeo.
Zaburi 23 : 5
5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
Matendo 16 : 23 - 34
Simulizi ya safari ya wana wa Israeli huongezewa thamani na bahari ya mshamu pamoja na jangwa na vikwazo vingi walivyokutana navyo.
Yoshua 2 : 9 - 11
Historia ya Daudi inapambwa na ushindi alioupata juu ya Goliath.
1 Samweli 18 : 6 - 7
Historia ya Danieli imepambwa na ushindi alioupata mbele ya adui zake waliomshitaki.
Danieli 6 : 23 - 26
Mhubiri: Mwl Ezekieli Malando
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com