Перейти к содержимому

MUMINA AWAWEZESHA AKINA MAMA NA WANABODABODA ISIOLO KUKUZA BIASHARA

𝐖𝐀𝐒𝐎 𝐓𝐕

0:00 / 0:00

MUMINA AWAWEZESHA AKINA MAMA NA WANABODABODA ISIOLO KUKUZA BIASHARA

479 просмотров · 1 мес. назад
𝐖𝐀𝐒𝐎 𝐓𝐕
7,31 тыс. подписчиков
479 просмотров · 1 мес. назад
Vikundi mbalimbali vya akina mama, waendeshaji wa boda boda na teksi, pamoja na mafundi wa bidhaa za chuma mjini Isiolo, vimepokea hundi za fedha kutoka kwa Afisi ya Mwakilishi wa Wanawake katika Kaunti ya Isiolo, Mumina Bonaya, kwa lengo la kuwawezesha kuimarisha shughuli zao za kiuchumi. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi hizo katika afisi yake, Mumina amesema kuwa maisha ya mwanadamu hayawezi kurejeshwa baada ya kupotea, akisisitiza umuhimu wa kulinda maisha ya wananchi. Mumina ametoa wito kwa viongozi wa Kaunti ya Samburu kuwa mstari wa mbele katika kutafuta suluhu ya kudumu ya kukomesha mauaji yanayohusishwa na ujangili, akisema juhudi zaidi zinahitajika ili kurejesha amani na usalama katika eneo hilo. Aidha, ametoa rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika shambulizi la Gotu, Kaunti ya Isiolo, akisema ataendelea kutetea usalama na haki ya kila mwananchi kuishi. Kwa mujibu wa Mumina, jumla ya vikundi 271 katika Kaunti ya Isiolo vimenufaika na mpango wake wa kuwawezesha wananchi kiuchumi katika kipindi cha miaka mitatu aliyokuwa madarakani. Aidha, Mumina amewakosoa wanaopinga mpango wake wa kusambaza taulo za usafi katika shule mbalimbali za wasichana, akisema mpango huo unalenga kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria masomo bila kukatizwa wakati wa hedhi kutokana na ukosefu wa bidhaa hizo muhimu. Naye Asha Abdirahman, mkazi wa Isiolo, ameunga mkono msimamo wa Gavana wa Isiolo, Abdi Ibrahim Hassan, pamoja na Mumina Bonaya wa kulaani mauaji yaliyotokea Gotu. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Jima ameunga mkono mkutano wa usalama unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, akisema viongozi na wadau wanapaswa kushirikiana kutafuta suluhu ya kudumu ya changamoto ya ukosefu wa amani katika eneo hilo. Naye Omar Godana amewakosoa viongozi kutoka Kaunti ya Narok kwa kile alichodai kuwa ni kutetea mauaji ya mifugo yanayofanyika Samburu Mashariki, huku wakipuuza mauaji ya wananchi yaliyotokea Gotu. Godana amesema viongozi wa Isiolo wameonyesha msimamo wa kutetea maisha na usalama wa wananchi wao, akitaka juhudi zaidi kuelekezwa katika kupata suluhu ya kudumu ya mzozo wa usalama katika eneo hilo. Join this channel to get access to perks:    / @wasotv   WASO TV - Informing and Entertaining