HII SIKU MVUA ILININYESHEA VIBAYA MNO KUANZIA SHAMBANI NA NJIANI MPAKA GHETO !!
Mapi
0:00 / 0:00
HII SIKU MVUA ILININYESHEA VIBAYA MNO KUANZIA SHAMBANI NA NJIANI MPAKA GHETO !!
26 просмотров · 2 ч назад
Mapi
2,75 тыс. подписчиков
26 просмотров · 2 ч назад
HII SIKU MVUA ILININYESHEA VIBAYA MNO KUANZIA SHAMBANI NA NJIANI MPAKA GHETTO KILOLO - IRINGA !!
NB: MSINISIKITIKIE WALA KUNIHURUMIA
Ilikua siku ya Jumapili, msimu wa mvua katika Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.
Ni kipindi ambacho shughuli za shamba zinakua zimepamba moto hasa kwa wakulima wa mazao kama Mahindi na parachichi.
Basi nami bila hiana na kwa ari nikaamua kuvaa boots zangu nikakamata Jembe na Panga nikatembea kama kilomita nne hivi kwenda kushughulikia mali shambani, - Miche michanga ya parachichi na Mahindi yalihitahi huduma yangu wakati huu.
Siku hii kulikua na game kali sana, moja ya ligi kuu Tanzania bara - Yanga SC Vs. Tabora United (ambapo uto alichapika kama sijakosea). Hii ilibidi tu inipite maana shughuli za shambani ni muhimu kuliko kuangalia mpira. Lakini pia ligi kuu uingereza palikua na game ya moto sana Kati ya Arsenal na Manchester City. Nilipanga pia nisiangalie (kama nisingepatwa na dhahama hii ya mvua) Ila baada ya mvua kuwa nyingi sana nililazimika kurudi maghetoni na baadae kwenda kucheki game ya Arsenal Vs. Man City.
Kilichotokea ni baada ya kufika shambani, nilianza kazi kama kawaida Ila baada ya masaa machache, mvua ikaanza kunyesha kidogokidogo, mi nlijipa moyo kwamba inavumilika nikaendelea kuhudumia mazao machanga shambani, Ila baadae mvua iliamua kuwa serious - Ikachapa kubwa huku ikiambatana na upepo na hapakua na nyumba ya kujificha karibu, so nilichapwa mvua vibaya mno, simu yangu ilikufa kutokana na kuloana sana!!
Nililazimika pia kuondoka mdogomdogo nikitembea huku mvua ikinichapa vibaya mno!! nikakatiza msitu wa kijiji nikafika maeneo ya vilabuni ambako kuna majengo na ningeweza kupumzima Ila kwakua tayari nilikua kama nimelowekwa hivi, nikaona wacha tu nimalizie safari mpaka maghetoni, Luganga, Mtitu - Kilolo Iringa, Tanzania - Africa.