ACT INAAMINI KATIBA MPYA INAWEZA KUPATIKANA KABLA YA UCHAGUZI WA 2030.- ADO
EastAfricaTV
0:00 / 0:00
ACT INAAMINI KATIBA MPYA INAWEZA KUPATIKANA KABLA YA UCHAGUZI WA 2030.- ADO
194 просмотра · 1 день назад
EastAfricaTV
1,25 млн подписчиков
194 просмотра · 1 день назад
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amehitimisha ziara yake katika Mkoa wa Kahama baada ya kukutana na wenyeviti na makatibu wa chama ngazi ya mikoa pamoja na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kagongwa.
Akizungumza na wananchi, Shaibu alisema anasikia kuna watu wanaosema haiwezekani kupata Katiba Mpya kwa sababu muda hautoshi, hivyo bora kuboresha tu Katiba ya sasa. Hata hivyo, yeye na chama chake wanaamini kuwa Katiba Mpya inaweza kupatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.