Tuhuma Dhidi ya Sheikh Rabii na Wanafunzi Wake | Kuhusu kurekodi Video | Wamemkhalifu Baada ya Kufa?
Manhaj Online TV
0:00 / 0:00
Tuhuma Dhidi ya Sheikh Rabii na Wanafunzi Wake | Kuhusu kurekodi Video | Wamemkhalifu Baada ya Kufa?
700 просмотров · 5 ч назад
Manhaj Online TV
13,7 тыс. подписчиков
700 просмотров · 5 ч назад
Je, ni kweli wanafunzi wa Sheikh Rabee' bin Hadi al-Madkhali wamemkhalifu na kugeuka baada ya kufa kwake, kuhusu kurekodi video (taswiir)?
Katika video hii muhimu, Sheikh Dr. Khamiis Imaam حفظه الله anaweka wazi uhalisia kuhusu tuhuma dhidi ya masheikh na madu'at wa Ahlus Sunnah. Je, Sheikh Rabee' alikuwa akilazimisha wanafunzi wake kufuata rai yake katika masuala ya khilaaf na ijtihad, au hayo ni maneno ya twa'an?
Yaliyomo:
• Majibu kuhusu Sheikh Munir as-Sa'adi, Sheikh Arafat al-Muhammadi, na Sheikh Abdullah al-Bukhari (Hafidhahumullah) - tangu lini walianza kurekodi video kwa ajili ya da'wah?
• Msimamo wa wanachuoni wakubwa kama Sheikh Ibn Uthaymeen na Sheikh Swaleh al-Luhaydan kuhusu kujuzu kwa tasweer kwa ajili ya maslahi ya da'wah.
• Mifano ya masuala khilafiyyah: Sheikh al-Albani na Sheikh Ibn Baz kuhusu hukumu ya anayeacha swala, na jinsi Sheikh Rabee' alivyomtetea Sheikh al-Albani dhidi ya tuhuma za Haddadiyyah.
• Sheikh Khalid ar-Raddadi, Sheikh Muhammad bin Ghalib al-Umari, na Sheikh Bandar al-Khaibari - ushahidi kuwa video zilikuwepo kabla na wakati wa uhai wa Sheikh Rabee'.
• Kutoa hadithi «...اتَّخذَ النَّاسُ رؤوسًا جُهَّالًا...» na kuzielekeza kwa masheikh na wanachuoni wa Sunnah wenye elimu.
Usikose kusikiliza hadi mwisho ili kupata ufahamu sahihi na kuepuka kuwavunjia heshima wanachuoni na wabebaji wa da'wah hii mubaaraka.
📌 Subscribe kwenye chaneli yetu ya Manhaj Online TV kwa darsa zaidi, mawaidha, na nasaha za kisheria. 🔔 Gusa kengele ili uwe wa kwanza kupata taarifa kila tunapoweka video mpya.