MFUGAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA MKINGA ANAVYONUFAIKA NA TEKNOLOJIA YA UPANDISHAJI KWA NJIA YA CHUPA
mkingadc digital
0:00 / 0:00
MFUGAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA MKINGA ANAVYONUFAIKA NA TEKNOLOJIA YA UPANDISHAJI KWA NJIA YA CHUPA
4 854 просмотра · 2 мес. назад
mkingadc digital
294 подписчика
4 854 просмотра · 2 мес. назад
Mhinduro, Mkinga – Tanga
Mfugaji wa kisasa wa ng'ombe wa maziwa, Bi. Dorice Charles Seif, mkazi wa Kijiji cha Mhinduro, Kata ya Mhinduro, Tarafa ya Maramba, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, ameendelea kuwa mfano wa mafanikio katika sekta ya mifugo baada ya kunufaika na teknolojia ya kisasa ya upandishaji wa ng'ombe kwa njia ya chupa (Artificial Insemination – AI).
Bi. Dorice anafuga jumla ya ng'ombe 18 wa maziwa, ambapo matumizi ya teknolojia hiyo yamechangia kupata mifugo yenye sifa bora za uzalishaji, kuongeza tija ya ufugaji na kuinua kipato cha familia yake.
Akielezea mafanikio aliyoyapata, amesema kuwa kabla ya kutumia teknolojia ya upandishaji kwa njia ya chupa alikuwa akizalisha wastani wa lita 2 hadi 3 za maziwa kwa siku. Hata hivyo, baada ya kutumia teknolojia hiyo, uzalishaji umeongezeka na kufikia lita 20 za maziwa kwa siku, jambo ambalo limemwezesha kuongeza kipato na kukidhi mahitaji ya soko.
Bi. Dorice amesema matarajio yake ni kuendelea kuboresha ufugaji wake kwa kushirikiana na wataalamu wa mifugo ili kuongeza uzalishaji na kufikia lita 60 za maziwa kwa siku, hatua itakayochangia zaidi kuinua uchumi wa familia yake na kuongeza upatikanaji wa maziwa bora kwa jamii.
Ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimarisha huduma za ugani na kusogeza teknolojia za kisasa za mifugo karibu na wafugaji, hatua inayowezesha kuongeza uzalishaji, kuboresha mifugo na kuinua maisha ya wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga inaendelea kuwahamasisha wafugaji kutumia teknolojia ya upandishaji kwa njia ya chupa pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalamu wa mifugo ili kuongeza uzalishaji wa maziwa, kuboresha ubora wa mifugo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kaya na Taifa kwa ujumla.
KaziNaUtuTunasongaMbele
#MkingayaMaendeleo
@samia_suluhu_hassan
@ikulu_mawasiliano
@owm_tz
@ortamisemi
@wizara_ya_kilimo
@mifugonauvuvi
@orvijana
@batilda.burian
@ofisiyamkuuwamkoawatanga
@mwakioja
@mkingadc