KATORO WALIVYOITIKIA KWA VITENDO ‘TONE TONE’ YA CHADEMA
Mwananchi Digital
0:00 / 0:00
KATORO WALIVYOITIKIA KWA VITENDO ‘TONE TONE’ YA CHADEMA
16 053 просмотра · 1 год назад
Mwananchi Digital
1,22 млн подписчиков
16 053 просмотра · 1 год назад
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche akiongoza kampeni ya kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za chama hicho maarufu kwa jina la 'Tone Tone' mara baada ya kuhitimisha hotuba yake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mji mdogo wa Katoro wilayani Geita.
Kupitia kampeni hiyo, Chadema inalenga kutoa fursa kwa kila mwenye mapenzi mema na mageuzi kuchangia kiasi chochote cha fedha anachojaaliwa sawa sawa na mapenzi yake.
Heche na viongozi wengine wa Kitaifa wa Chadema wako kwenye ziara ya kampeni ya 'No reforms, No election' inayoendelea katika mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza inayounda Kanda ya Victoria kwa mfumo wa chama hicho.