MAAGIZO YA CCM TANGA: KWAGILWA AWASWEKA NDANI VIONGOZI WA JIJI KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA USAFI
Millard Ayo
0:00 / 0:00
MAAGIZO YA CCM TANGA: KWAGILWA AWASWEKA NDANI VIONGOZI WA JIJI KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA USAFI
5 164 просмотра · 1 день назад
Millard Ayo
6,21 млн подписчиков
5 164 просмотра · 1 день назад
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe Reuben Kwagilwa ameagiza kukamatwa na kuhojiwa Kaimu Afisa Biashara wa Jiji la Tanga Hussein Mbwana, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Bahati Kahindi na meneja wa soko la Mgandini kwa kushindwa kusimamia usafi wa masoko.
Hatua hiyo imekuja baada ya agizo la Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Kenani Kihongosi alilolitoa Septemba 26,2026 katika ziara yake mkoani Tanga na kusema kuwa usafi wa Jiji hauridhishi hivyo hatua za haraka zichukuliwe.
Katika ziara ziara yake Jijini Tanga Mhe Kwagilwa ametembelea masoko yote kukutana na changamoto ya kukosekana vyoo vya uhakika,kuziba mifereji,utiririshaji wa maji taka na kutozolewa taka kwa wakati ambapo katika mahojiano wahusika walishindwa kumpa majibu na kuagiza wakamatwe.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian awali amesema alishatoa maelekezo kuhusu suala la usafi ikiwemo wananchi kuchukuliwa hatua ila bado hakuna utekelezaji uliofanyika.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Daddy Kolimba amesema kamati ya ulinzi na usalama ilifanya ziara na kukagua baadhi ya maeneo hayo na walitoa maelekezo ili inaonekana hakuna utekelezaji.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mbunge wa Tanga Mjini kwa sasa ni Kassimu Mbaraka amesema ziara hiyo inaweza kuwa na manufaa kwa masrahi ya wananchi wa jiji la Tanga.