TAHARUKI MONDULI! WANANCHI WALIA WENZAO KUWA MAHABUSU SIKU 20 KWA KUMZUIA MWEKEZAJI KUVUNJA NYUMBA..
Global TV Online
0:00 / 0:00
TAHARUKI MONDULI! WANANCHI WALIA WENZAO KUWA MAHABUSU SIKU 20 KWA KUMZUIA MWEKEZAJI KUVUNJA NYUMBA..
3 670 просмотров · 12 часов назад
Global TV Online
5,98 млн подписчиков
3 670 просмотров · 12 часов назад
TAHARUKI MONDULI! WANANCHI WALIA WENZAO KUWA MAHABUSU SIKU 20 KWA KUMZUIA MWEKEZAJI KUVUNJA NYUMBA ZAO
Taharuki kubwa imeendelea kutanda katika Kitongoji cha Saburi, kilichopo Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, kufuatia sintofahamu ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji anayedaiwa kutaka kubomoa makazi yao.
Katika ripoti hii maalum ya Global TV Online, wananchi na akina mama wanalia kwa uchungu wakieleza jinsi kundi la watu waliokuwa na silaha za jadi na tingatinga (katapila) walivyovamia kijiji hicho kwa lengo la kuvunja nyumba zao kabla ya wananchi kujitokeza kuzuia zoezi hilo. Hali hiyo imepelekea baadhi ya wakazi kukamatwa na kushikiliwa mahabusu kwa zaidi ya siku 20 bila kufikishwa mahakamani, huku wengine wakiishi mafichoni kwa hofu ya kukamatwa.
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com