Перейти к содержимому

WACHIMBAJI WA MADINI SAZA WAPATIWA ELIMU YA VVU NA MATUMIZI YA KINGA

Damian online Tv

0:00 / 0:00

WACHIMBAJI WA MADINI SAZA WAPATIWA ELIMU YA VVU NA MATUMIZI YA KINGA

54 просмотра · 2 нед. назад
Damian online Tv
39 подписчиков
54 просмотра · 2 нед. назад
Ofisi ya TACAIDS nyanda za juu kusini ,ikiongozwa na EMMANUEL PETRO-mchumi mkuu wa TACAIDS kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya songwe ,,uongozi wa serikali za kata , vituo vya afya watoa huduma ngazi ya jamii wamefikia wachimbaji wa madini wapatao 880 pamoja na wamiliki zaidi ya migodi saba kwa kutoa elimu ya masuala ya VVU , na UKIMWI elimu ya mahusiano ya magonjwa na ngono na maambukizi ya VVU ,elimu sahihi ya matumizi ya kondomu kusambaza kondomu zaidi 11,800 kwa wachimbaji katika migodi ya saza katika halmashauri ya wilaya ya songwe mkoa wa songwe Aidha elimu hii imetoa hamasa kubwa wa jamii ya wachimbaji wa madini kuzitumia huduma za ukimwi kama upimaji wa VVU ,dawa kinga [prEP] jipime [HIV Self-test] na kuanzisha vituo vya kusambazia kondomu katika maduara ya uchimbaji kwa ajiri ya kujikinga na maambukizi ya VVU na magonjwa ya ngono kwa wachimbaji Baada ya elimu ya UKIMWI kwa wachimbaji ,TACAIDS imeshauri Halmashauri kwa kuwatumia watoa huduma wa afya toka katika vituo vya afya vinavyozunguka migodi kufanya huduma mkoba ya upimaji wa VVU, na kusambaza vipimio vya jipime katika migodi yote ikiwa ni sambamba na usambazaji wa kondomu kwa wachimbaji katika migodi yote. Wamiliki wa migodi pamoja na vijana wanaojihusisha na uchimbaji wafurahia sana kufikiwa na elimu ya masuala ya UKIMWI kwa wachimbaji pamoja na jamii zinazowazunguka kuimarisha katika uchimbaji wa madini ambayo ndiyo shughuri zao kubwa za kiuchumi na ngu hivyo elimu hiyo imeenda kuwafungua huku wakikabidhiwa kondomu na wakiahidi kujiepusha na ngonozembe . #damiantv #creativemedianews #newaupdate #songwemkwajuni #dunia #chunyambeya