BABA, NINATAKA KUOLEWA…. NISAIDIE! - Sehemu ya KWANZA | Pastor James Kalekwa
Pastor James Kalekwa
0:00 / 0:00
BABA, NINATAKA KUOLEWA…. NISAIDIE! - Sehemu ya KWANZA | Pastor James Kalekwa
746 просмотров · 3 г. назад
Pastor James Kalekwa
2,53 тыс. подписчиков
746 просмотров · 3 г. назад
Ninafundisha somo hili kama majibu kwa binti wa kufikirika ambaye amekuja ofisini kwangu akiwa amesikia mengi sana ambacho yamemchanganya… lakini hajasikia NENO LA MUNGU linasemaje. Binti anakuja ofisi ya mchungaji akiwa kwenye machozi mengi na kilio chake ni hiki “BABA, NINATAKA KUOLEWA…. NISAIDIE!”
1. Ndoa imeasisiwa na Mungu. Hii ni taasisi iliyotengenezwa na Mungu mwenyewe ambayo pamoja na mambo mengine, hatimaye impe utukufu Yeye mwenyewe. (Ndiyo kutakuwa na maswala ya kufurahiana, kukamilishana, kutoshelezani, kuzaa, kulea n.k)
“BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
Mwa 2:18, 23-24 SUV
#ndoa #jameskalekwa #babanisaidie