Yesu Kristo, Roho Mtakatifu (Mathayo 28:16-20)
Saganga Kapaya
0:00 / 0:00
Yesu Kristo, Roho Mtakatifu (Mathayo 28:16-20)
239 просмотров · 4 года назад
Saganga Kapaya
69 подписчиков
239 просмотров · 4 года назад
#Mungu #Kristo #Yesu
"Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma" Yohana 17:3.
Video hii inafafanua kile ambacho Biblia inafundisha kuhusu Mungu na Mwana wake wa Pekee Yesu Kristo.
Karibu usikilize kile ambacho Biblia inasema kuhusu Mungu. Waweza pia kupitia mafungu yafuatayo na kutafakari juu ya Mungu na Kristo. Mwanzo 1:1, Yohana 1:1, Waefeso 4:5-6, 1 Wakorintho 8:6, 1 Timotheo 2:5, Ufunuo 1:1-2. Pia waweza kupitia utangulizi wa kila kitabu au waraka wa Biblia kuanzia mafungu matano tu ya mwanzo, utaona jinsi ambavyo Biblia inavyomfunua Mungu na Yesu kuwa ni akina nani, kinyume kabisa na wengi walivyozoea kumfafanua.
Katika utume kwa wanafunzi wake, Kristo sio tu aliorodhesha kazi yao, lakini aliwapa ujumbe wao. Wafundisheni watu, alisema, “kuyashika yote niliyo waamuru ninyi.” Wanafunzi walipaswa kufundisha kile Kristo alichofundisha. Kile alichokitamka, siyo tu yeye katika nafsi, bali kupitia manabii wote na waalimu wa Agano la Kale, hapa wamejumuishwa. Fundisho la binadamu limefungiwa nje. Hakuna nafasi kwa ajili ya pokeo, kwa ajili ya nadharia na mahitimisho ya kibinadamu, au kwa ajili ya sheria ya kanisa. Si moja ya haya watumishi wa Kristo wanapaswa kufundisha. “Sheria na manabii,” pamoja na kumbukumbu ya maneno yake mwenyewe na matendo, ni lulu walizokabidhiwa wanafunzi kwa ajili ya kutolewa kwa ulimwengu. Jina la Kristo ndiyo neno-kuu lao, nembo yao ya kujitofautisha, kifungo cha umoja, mamlaka kwa ajili ya njia ya utendaji wao, na chanzo cha mafanikio yao. Hakuna kitu kisichokuwa na muhuri wake kinachopaswa kutambuliwa katika Ufalme wake. [Tumani la Vizazi Vyote, uk.826]/ [The Desire of Ages, p.826]
“Na waende kwa sheria na ushuhuda: ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isaya 8:20. Watu wa Mungu wameelekezwa katika Maandiko kama ulizi wao dhidi ya ushawishi wa waalimu wa uongo na nguvu idanganyayo ya roho za giza. Shetani kila mbinu inayowezekana kuwazuia watu kupata ujuzi wa Biblia; kwa kuwa matamshi yake ya wazi yanashihirisha uongo wake. Katika kila uamsho wa kazi ya Mungu mfalme wa uovu ameamushwa kufanya kazi zaidi; sasa anaweka juhudi zake zote kwa ajili ya pambano la mwisho dhidi ya Kristo na wafuasi wake. Uongo mkuu wa mwisho punde utafunuliwa mbele zetu. Mpinga-kristo atatenda kazi zake za ajabu katika macho yetu. Kwa ukaribu sana iliyobandia itafanana na iliyo kweli kiasi kwamba itakuwa haiwezekani kuzitofautisha isipokuwa kwa Maandiko Matakatifu. Kwa ushuhuda wao kila sentensi na kila muujiza ni lazima upimwe. [Pambano Kuu, uk.593]/[The Great Controversy, p.593]
Lakini Mungu atakuwa na watu juu ya dunia kwa ajili ya kuisimamia Biblia, na Biblia pekee, kama kipimo cha mafundisho yote na msingi wa matengenezo yote. Mapendekezo ya watu wasomi, wajumuisho ya sayansi, kanuni au maamuzi ya mabaraza ya kikanisa, kama yalivyo mengi na yasiyopatana kama yalivyo makanisa wanayoyawakilisha, sauti ya wengi – siyo moja wala yote ya haya yanayopaswa kudhaniwa kama Ushahidi kuunga au kupinga kitu chochote cha imani ya kidini. Kabla ya kukubali fundisho au kanuni yoyote, ni lazima tudai lilizo wazi “ Hivi ndiyo asema Bwana” kuliunga mkono.
Shetani anadumu akidiriki kushawishi watu wamtazame mtu badala ya Mungu. Anawaongoza watu kuwatazama makasisi, wachungaji, maprofesa wa teologia, kama miongozo yao, badala ya kuyachunguza Maandiko ili kujifunza wajibu wao wenyewe. Ndipo, kwa kuzidhibiti akili za hawa viongozi, anaweza kuwashawishi makutano kwa kadri atakavyo. [Pambano Kuu, uk.595]/[The Great Controversy, p.595]
“Heri wenye njaa na kiu ya haki; maan hao watashibishwa.” – Matayo 5:6.
Haki ni holiness, kufanana na Mungu, na “Mungu ni upendo.” 1 Yohana 4:16. Ni kufungamana na sheria ya Mungu, kwa kuwa “amri [maagizo] yako yote ni haki.” (Zaburi 119:172), na “pendo ndilo utimilifu wa sheria”. (Warumi 13:10). Haki ni upendo, na upendo ni nuru na uzima wa Mungu. Haki ya Mungu iko ndani ya Kristo. Tunapokea haki kwa kumpokea yeye.
Siyo kwa bidii zenye maumivu au kazi za kujitaabisha, siyo kwa zawadi au kafara, haki hupatikana; lakini hutolewa bure kwa kila nafsi yenye njaa na kiu ya kuipokea. “Haya, kila aonaye kiu, njooni majini, Naye asiye na fedha; njooni, nunueni mle, … bila fedha na bila thanani,” Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana” na, “na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.” Isaya 55:1; 54:17; Yeremia 23:6.
Hakuna mjumbe wa kibinadamu anayeweza kutoa kile kinachoweza kukidhi njaa na kiu ya nafsi. Lakini Yesu anasema, “Tanzama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” “Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.” Ufunuo 3:20; Yohana 6:35. [Mlima wa Baraka, uk.18-19]/[Thoughts from the Mount of Blessing, p.18-19]
Kwa mawaasiliano zaidi : tenaimeandikwa@gmail.com, +255 716 236 149