Перейти к содержимому

Mbunge Mwanyika: Atoa Somo kwa wakulima wa parachichi njombe kuongeza uzalishaji kupitia ufugaji

Mchuchuma tv

0:00 / 0:00

Mbunge Mwanyika: Atoa Somo kwa wakulima wa parachichi njombe kuongeza uzalishaji kupitia ufugaji

255 просмотров · 7 месяцев назад
Mchuchuma tv
8,59 тыс. подписчиков
255 просмотров · 7 месяцев назад
Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deo Mwanyika, amewataka wakulima wa zao la parachichi kuanza kufuga mifugo mbalimbali ili kuwasaidia kuzalisha samadi kwa ajili ya kuboresha rutuba ya mashamba yao. Akizungumza katika ziara yake ya kikazi iliyofanyika Februari 5, 2026, mbunge huyo alisema kuwa matumizi ya samadi kwenye miche ya maparachichi yataongeza kiwango cha uzalishaji wa matunda na kuboresha ubora wake. Alisisitiza kuwa kilimo cha kisasa kinahitaji mbinu endelevu zikiwemo matumizi sahihi ya mbolea za asili. Mwanyika alieleza kuwa Jimbo la Njombe Mjini ndilo kitovu kikubwa cha uzalishaji wa parachichi katika Mkoa wa Njombe, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kuimarisha sekta hiyo kwa kuongeza uzalishaji pamoja na kujenga viwanda vya kuchakata parachichi ili kuongeza thamani ya zao hilo na kufungua fursa zaidi za ajira kwa vijana. Ameyasema hayo alipokuwa katika Shule ya Msingi Omago, alikofanya shughuli maalum ya upandaji wa miti 200 ya parachichi ambayo ni mali ya shule hiyo. Hatua hiyo inalenga kuhamasisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kushiriki katika kilimo cha parachichi na kutambua umuhimu wake kiuchumi na katika maswala mazima ya lishe Bora kwa wanafunzi. Mbunge huyo amewahimiza wakulima kuendelea kushirikiana na wataalamu wa kilimo ili kuhakikisha wanatumia mbinu bora zitakazowawezesha kuongeza uzalishaji na kipato chao kupitia zao la parachichi.