Перейти к содержимому

🔴TRA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YAVUKA LENGO LA UKUSANYAJI KODI, Tsh. 231B ZAKUSANYWA

RUVUMA TV

0:00 / 0:00

🔴TRA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YAVUKA LENGO LA UKUSANYAJI KODI, Tsh. 231B ZAKUSANYWA

159 просмотров · 2 нед. назад
RUVUMA TV
76,9 тыс. подписчиков
159 просмотров · 2 нед. назад
Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inayojumuisha Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Rukwa, Katavi na Ruvuma imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 121 katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, baada ya kukusanya shilingi bilioni 231 dhidi ya lengo la shilingi bilioni 190.144. Akitoa taarifa hiyo katika ufunguzi wa kikao cha robo ya kwanza cha viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kilichofanyika mkoani Ruvuma, Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma, Sylver Rutagwelera, amesema makusanyo hayo yanaonesha ukuaji wa asilimia 32 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha 2025/2026. Amesema mafanikio hayo yametokana na sera na sheria za ukusanyaji kodi zilizowekwa na Serikali, usimamizi na utekelezaji wake unaofanywa na viongozi pamoja na watumishi wa TRA, sambamba na mshikamano, uzalendo na ushirikiano mzuri kati ya wafanyabiashara na mamlaka hiyo. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa katika ufunguzi wa kikao hicho, amewapongeza viongozi wa TRA kwa kusimamia utekelezaji wa sera na sheria za kodi na kufanikisha kuvuka lengo la makusanyo lililowekwa. Aidha, amewataka viongozi na watumishi wa TRA kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za ukusanyaji kodi. Akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na wafanyabiashara, kutoa elimu ya kodi na kutatua changamoto zinazowakabili ili kuongeza uelewa na kuwahamasisha kulipa kodi kwa hiari.