Перейти к содержимому

DKT. KIKWETE AKAGUA MATUNDA YA JAMII SALAMA,KUTOKA KLINIKI TEMBEZI HADI ZAHANATI,

Cg Online Tv

0:00 / 0:00

DKT. KIKWETE AKAGUA MATUNDA YA JAMII SALAMA,KUTOKA KLINIKI TEMBEZI HADI ZAHANATI,

158 просмотров · 1 день назад
Cg Online Tv
97,4 тыс. подписчиков
158 просмотров · 1 день назад
#CgOnlineTv #DKTKIKWETE Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, anaendelea na ziara ya siku nne mkoani Tabora, iliyoanza Septemba 12, 2026, ambapo pamoja na mambo mengine anakagua miradi ya afya inayotekelezwa na JMKF. Katika ziara hiyo, Dkt. Kikwete anatembelea na kukagua zahanati zilizojengwa kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa zaidi ya wakazi 36,000 katika vijiji viwili vya pembezoni na jamii zinazovizunguka katika wilaya za Sikonge na Uyui. Leo Septemba 13, 2026, kabla ya kukagua zahanati pamoja na nyumba mbili za wafanyakazi zilizopo katika Kitongoji cha Ipembe, Kata ya Kiloli, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Dkt. Kikwete amekagua mradi wa kliniki tembezi wa Jamii Salama katika eneo hilo. Mradi huo wa Jamii Salama uliendeshwa na JMKF mwanzoni mwa mwaka 2025 kupitia kliniki tembezi, ambapo mamia ya wanawake wajawazito walipatiwa huduma muhimu za afya bila malipo. Baada ya kuona ukubwa wa mahitaji ya huduma hizo, JMKF iliamua kujenga zahanati hizo pamoja na nyumba za wafanyakazi ili kuweka msingi wa huduma za afya za kudumu kwa jamii zilizo mbali na vituo vya afya vya wilaya na mkoa. Kwa upande wao, wananchi wa Kitongoji cha Ipembe wameishukuru JMKF kwa kuwasaidia kusogeza huduma za afya karibu na makazi yao, wakieleza kuwa hapo awali walilazimika kusafiri zaidi ya kilomita 20 kwenda kijiji kingine kutafuta huduma za afya. Wananchi hao wamesema hali hiyo ilikuwa ikiwalazimu kutumia fedha nyingi kwa usafiri, huku baadhi yao wakishindwa kufika kliniki kwa wakati, jambo walilodai lilichangia vifo vya baadhi ya wanawake wajawazito. Kesho Septemba 14, 2026, Dkt. Kikwete anatarajiwa kuelekea Wilaya ya Uyui, ambapo atatembelea na kukagua zahanati pamoja na nyumba mbili za wafanyakazi zilizopo katika Kijiji cha Gengesita, Kata ya Kizengi.