Abdillah albakeer- NAJUTA - (official nasheed video )
Abdillah Albakeer
0:00 / 0:00
Abdillah albakeer- NAJUTA - (official nasheed video )
871 просмотр · 3 дн. назад
Abdillah Albakeer
548 подписчиков
871 просмотр · 3 дн. назад
munsheed Abdillah albakeer
our contact +255685518429
Abdullahabuuubakr@gmail.com
LYRICS
Siku nyingi zimepita mambo mengi metendeka
Ya furaha tulipata na mabaya kutufika
kwa makosa tulikwenda kwenye kumuasi muumba
Tukaona ndo kupata leo hii twayajuta
Naapa mimi najuta nilipokua nasuka
Na tatuu kubandika na hazitaki kutoka
Mziki niliufuata mbali pia nilifika
Nikawa natoa pesa wanawake kuwapata
Najuta sana najuta mola wangu kumkosa
Natamani kutoroka kabla ya kwake kufika
Wapi ataponiweka roho yangu ikitoka
Mola wangu naogopa nisamehe kwa hakika
Swala zilinipita na swaumu kizikosa
Magetoni kujificha na chakula kukipika
Tukala huku twacheka na sigara kuzivuta
kweli rafiki si kaka anaweza kukutupa
Yamebaki kwenye kichwa yote tuliyoyafanya
Natamani kuyaficha ila moyo unakana
Mbele yako nikifika yote yataonekana
Najuta rabbi najuta takuwaje kiniona
Mengi siwezi yasema mola wangu wayajua
Ninachoomba salama mbele yako kisimama
Mola mwingi wa huruma msamehevu wa umma
Hatuna pengine bwana kwako wewe twarejea
Yote haya ni mjuto siwezi rejea tena
Nifikapo kwako Allah nitunuku yako janna
Unipe nguvu ya roho nyuma kamwe sirejee
kwako wewe najutia msamehevu pekee.