Перейти к содержимому

RC MTAKA AZUNGUMZA NA WAKULIMA WA MAHINDI KUHUSU BEI NA UHIFADHI

Mchuchuma tv

0:00 / 0:00

RC MTAKA AZUNGUMZA NA WAKULIMA WA MAHINDI KUHUSU BEI NA UHIFADHI

1 638 просмотров · 11 ч назад
Mchuchuma tv
8,4 тыс. подписчиков
1 638 просмотров · 11 ч назад
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amekutana na wakulima wa zao la mahindi kutoka Wilaya ya Ludewa kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya namna ya kutatua changamoto ya masoko pamoja na ukosefu wa maghala ya kuhifadhia mazao, lengo likiwa ni kumwezesha mkulima kunufaika zaidi na kilimo. Kilio kikubwa cha wakulima hao ni kukosekana kwa masoko ya uhakika na bei zinazokidhi gharama za uzalishaji, ambazo wanazitaja kuwa ni kubwa. Wakulima hao wanasema kwa ekari moja hutumia zaidi ya shilingi milioni moja katika uzalishaji wa mahindi. Hata baada ya kuzalisha, wakulima hao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maghala ya kuhifadhia mahindi, hali inayowatia hofu kutokana na taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa kuhusu uwepo wa mvua za El Niño. Kikao hicho kimehusisha baadhi ya wakulima pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe na Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, ambapo wamebadilishana mawazo kuhusu namna ya kupata suluhisho la pamoja la changamoto hizo. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuharakisha mchakato wa kuwakaribisha wawekezaji watakaoweza kujenga maghala kwa ajili ya kuhifadhi mahindi, pamoja na kuwakaribisha wawekezaji katika sekta ya viwanda vya kuongeza thamani ya zao hilo. Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema anaenda kufanya mpango wa kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, Daniel Vhongo, ili kuona namna ya mahindi ya wakulima wa Ludewa yanavyoweza kununuliwa kabla ya kuanza kwa mvua za El Niño, hatua inayolenga kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mazao hayo kukosa mahali salama pa kuhifadhiwa. 🔥 Niandikie hapa chini ulichojifunza kutoka kwenye video hii. 🙏 Asante sana kwa kuendelea kuwa mwanafamilia wa Mchuchuma TV. 💬 Usisahau kutoa maoni, na kuisambaza kwa wengine. wasiliana nasi kupitia 0628710325 Jina langu Maiko Saston Mwamlima