KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI YAELEKEZA MIRADI KULETA TIJA KWA WANANCHI KAHAMA
Mwananchi Digital
0:00 / 0:00
KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI YAELEKEZA MIRADI KULETA TIJA KWA WANANCHI KAHAMA
485 просмотров · 1 день назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
485 просмотров · 1 день назад
Kahama. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imeielekeza serikali mkoani Shinyanga kuhakikisha miradi ya maendeleo inayopelekwa mkoani humo inawanufaisha wananchi wa kipato cha chini ili kukuza uchumi wao.
Akizungumza leo oktoba 18,2026, wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa kwa ufadhili wa benki ya dunia kupitia mradi wa uendelezaji miji ya Tanzania (Tactic), wilayani Kahama, mwenyekiti wa kamati, Florent Kayombo, ameelekeza miradi hiyo kukamilishwa kwa wakati ili ilete tija kwa wananchi.
Amesema “Miradi hii wakati inajengwa kuna wananchi waliokuwa wanatoa huduma katika mazingira ambayo hayakuwa katika kiwango kinachotakiwa, tunaomba viongozi wetu wa mkoa na wilaya, mhakikishe wale wenyeji wa maeneo yote wanapewa kipaumbele. Tamisemi tunaomba fedha mkandarasi alipwe.”
Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi, John Cheyo, amesema Serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Kahama, akiwahakikishia wakandarasi kuwa fedha za kuwalipa zipo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Pili Mnyema, amesema “Tumejipanga vizuri kuhakikisha miradi yote inayoendelea inakamilika kwa wakati, kuna miradi mingi ya kimkakati, tupo tayari kuendelea kuisimamia na maelekezo yote tutayatekeleza.” Amesema Mnyema.gesi zaidi.