Перейти к содержимому

SUK NI MFUMO WA KUUNGANISHA NGUVU NA MAWAZO KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR

Ofisi ya Makamu Wa Kwanza wa Rais Zanzibar

0:00 / 0:00

SUK NI MFUMO WA KUUNGANISHA NGUVU NA MAWAZO KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR

1 406 просмотров · 5 дн. назад
Ofisi ya Makamu Wa Kwanza wa Rais Zanzibar
275 подписчиков
1 406 просмотров · 5 дн. назад
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman leo Septemba 30, 2026, amewasili ofisini kwake, kuendelea na majukumu ya kazi. Mheshimiwa Othman ameshika wadhifa huo wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi, Septemba 22 mwaka huu. Hafla hio ya kuwasili na mapokezi, iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Migombani, Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja, imewajumuisha watumishi wa Idara zote na sekta zilizopo katika Ofisi hio, zikiwemo Sekta ya Mazingira, Tume ya Ukimwi Zanzibar, Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu, Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya, Idara Mipango na Sera, Utumishi na uendeshaji, Faragha na ofisi kuu Pemba. Viongozi mbali mbali wamejumuika katika hafla hio wakiongozwa na Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe Hamza Hassan Juma na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Bi. Maryam Juma Abdallah.