BAMIA 10 kila siku kwa siku 21 mfululizo! TEGEMEA HAYA
Mshani Wellness
0:00 / 0:00
BAMIA 10 kila siku kwa siku 21 mfululizo! TEGEMEA HAYA
14 380 просмотров · 9 месяцев назад
Mshani Wellness
102 тыс. подписчиков
14 380 просмотров · 9 месяцев назад
Hizi hapa Faida za Bamia ikiwa utatumia bamia 3 kila siku kwa siku 10 mfululizo
Inatibu tatizo la kupata choo ngumu.
Bamia ina kiwango kikubwa cha Ufumwe au nyuzinyuzi ambazo husaidia kuimarisha afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
Mbali na kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi, bamia pia ina kiwango kikubwa cha kemikali ya mucilage ambayo husaidia kuimarisha mjongeo wa misuli ya tumbo
Inatibu magonjwa ya moyo na kukulinda ikiwa upo katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo.
Bamia ni msaada mkubwa kwao kwasababu, kiwango cha quercetin na rutin ndani ya bamia kinatosha kuufanya mmea huu kuwa miongoni mwa mimea yenye msaada mkubwa katika kuimarisha afya ya moyo.
Kupunguza uzito
Mbali na ndizi bamia pia inasaidia kukufanya ujihisi umeshiba kwa muda mrefu, kwa hivyo inakuepusha kula chakula kingi zaidi. Na kukusaidia kupunguza uzito bila shuruti ya kuchagua vyakula
Kuimarisha afya na muinekano wa ngozi
Bamia ina kemikali za catechins and epicatechins ambao husaidia kuondoa sumu za mwili ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kuzeeka kwa ngozi.
Inasaidia kuimarisha kinga ya mwili.
Bamia ni miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin C, Zinc na glutathione. Kemikali hizi husaidia kuimarisha kinga na kukukinga na maradhi mbalimbali ya mwili.
Ni chakula cha muhimu kwa wenye kisukari
Vyakula vyenye nyuzinyuzi husaidia kurekebisha sukari ya mwili kwa kuimarisha muitikio wa homoni za insulin ambazo ndio hurekebisha kiwango cha sukari katika damu.
Bamia ni miongoni mwa vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi, kwa hivyo matumizi ya bamia hukusaidia kuleta nafuu kwa wagonjwa wa kisukari lakini pia kukukinga na ugonjwa huu.
Inaimarisha afya ya ubongo na kuongeza kumbukumbu
Bamia ni chanzo kizuri cha folic acid, virutubisho ambavyo husaidia kuimarisha utendaji kazi wa ubongo.