Перейти к содержимому

Mchungaji Silvanus azikwa, aliacha ujumbe kwa mama yake

Mwananchi Digital

0:00 / 0:00

Mchungaji Silvanus azikwa, aliacha ujumbe kwa mama yake

16 046 просмотров · 1 месяц назад
Mwananchi Digital
1,22 млн подписчиков
16 046 просмотров · 1 месяц назад
Mwanga. Mchungaji Silvanus Msuya(44) amezikwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), usharika wa Shighatini, Dayosisi ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro huku akiacha kitabu maalumu kwa mama yake mzazi, Haika Msuya alichokipa jina la "Chozi la mama". Imeelezwa lengo la kitabu hicho ni kumpa heshima mama yake na kuonyesha ni kwa namna gani alimpambania licha ya changamoto alizopitia. Katika mazishi hayo yaliyofanyika leo Julai 30, 2026 vilio na simanzi vilitawala huku baadhi ya mamia ya waombolezaji walioshiriki mazishi hayo wakizimia na wengine wakibubujikwa machozi. Mchungaji Silvanus Msuya alifariki dunia Julai 26, 2026 katika Hospitali ya Rabininsia jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na tatizo la kupumua lililopelekea kifo chake. Novemba 3, 2024 Mchungaji Silvanus alibarikiwa kuwa Mchungaji wa Dayosisi ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro na amekuwa Mchungaji kiongozi Usharika wa Spillway Jimbo la Tambarare na Mchungaji Mwenza Usharika wa kanisa kuu Mwanga na Mratibu wa habari na mawasiliano Dayosisi ya Mwanga. Akitoa salamu za rambirambi, Mchungaji wa kanisa la KKKT, Usharika wa Kijitonyama, Dk Eliona Kimaro amesema Mchungaji Silvanus ameacha kitabu ambacho ameandika kwa heshima ya mama yake na kukiita "Chozi la mama". "Hii ni kuheshimu namna ambavyo mama kwa maombi yake ya umama ameweza kumlea na kumtengeneza mpaka hapo alipofikia.Tuendelee kupata hicho kitabu ambacho ni chake cha mwisho na huu ndio urithi mzuri aliotuachia na kuwatia moyo wanawake wote wawaombee watoto wao,"amesema Mchungaji Kimaro Aidha, amesema kanisa hilo litamkumbuka Mchungaji Silvanus kwa namna ambavyo alitumika katika kanisa hilo kwa kutoa ushuhuda wa maisha yake aliyopitia kuwasaidia vijana na wanawake katika sharika alizohudumu. " Mchungaji ametuhudumia katika ibada mbalimbali za Jumapili, amekuwa mwalimu lakini ameendesha programu mbalimbali za ‘counseling’ (ushauri nasaha) akiwasaidia sana watu ambao wamepata shida ya pombe kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ambao kwa kiasi kikubwa aliwabadilisha.”