Перейти к содержимому

DARSA: الجامع لعبادة الله وحده 🔴DARSA: Kutarajia والرجاء na Kutawakali والتوكل. Ust Ali bin Masoud

Darsa na Mihadhara

0:00 / 0:00

DARSA: الجامع لعبادة الله وحده 🔴DARSA: Kutarajia والرجاء na Kutawakali والتوكل. Ust Ali bin Masoud

18 просмотров · 7 дней назад
Darsa na Mihadhara
863 подписчика
18 просмотров · 7 дней назад
Darsa ilifanyika Rabi'ul Awwal 23, 1448 H Jumamosi Septemba 05, 2026 الجامع لعبادة الله وحده Al Jaami'u (Kusanyo lenye Kuhusiana na) Ibada kwa Ajili ya Allah Pekee Kutarajia/Tarajia (kuwa na matumaini ya kupata heri) والرجاء من أنواع العبادة الرجاء : وهو تأميل الخير فيما لا يقدر عليه إلا الله Katika aina za ibada ni Kutarajia: nako ni kutarajia heri (yaani:kuwa na matumaini ya kupata heri) katika yale mambo ambayo kwayo hakuna ayawezae mambo hayo isipokuwa Allah Pekee. فلا يجوز أن ترجو غير الله فيما لا يقدر عليه إلا الله Hivyo basi haijuzu hairuhusiwi kumtumainia yeyote mwengine isiyekuwa Allah katika yale mambo ambayo hakuna ayawezae isipokuwa Allah Pekee. Ama kuhusiana na kumtarajia mtu katika mambo ya kawaida أما الرجاء في الأمور العادية كأن ترجو من شخص أن يعطيك مالاً أو يساعدك فيما يقدر عليه kama vile kutarajia kwamba mtu atakupa mali au kukusaidia katika yale ambayo anayaweza kufanya; hii halina ubaya kwa kuwa si katika Ibada فهذا ليس من العبادة تقول : يا أخي، أرجوك أن تعطيني كذا وكذا، مما يقدر عليه Unaweza kusema: Ewe ndugu yangu! nakuomba unipe kadha na kadha, ukimaanisha katika yale mambo ambayo anayaweza kufanya. لكن لا ترج مخلوقا فيما لا يقدر عليه إلا الله walakini usimtarajie mahuluku yoyote yule katika yale ambayo hakuna ayawezae isipokuwa Allah Pekee. كالذين يرجون الأموات والغائبين والجن، هذا يجوز، وهو شرك أكبر Kama wale wanaowatarajia wenye kuweka matumaini yao wafu, na wasiokuwepo, na majini; hili halijuzu haliruhusiwa nalo ni shirki kubwa. Tawakali (Kutawakali/kutegemea) والتوكل من أنواع العبادة التوكل : وهو تفويض الأمور إلى الله الاعتماد عليه Tawakali ni katika aina za Ibada nako ni kuyafawidhi mambo yote kwa Allah kumtegemea ambayo ni kumkabidhi Mungu mambo na kumtegemea. Amesema Ibn Rajab katika kufafanua Tawakati :قال ابن رجب في تعريف التوكل هو صدق اعتماد القلب على الله عز وجل في استجلاب المصالح Tawakuli ni: ukweli wa muegemeo uwegemeaji wa moyo kuegemea kwa Allah katika kuleta mambo yenye maslahi na manufaa. ودفع المضار من أمور الدنيا والآخرة كلها Na kuepusha kujikinga na madhara katika mambo ya kidunia na Akhera وكِلَةُ الأمور كلها إليه Na kuyaegemeza mambo yote Kwake (yaani: Allah Pekee) وتحقيق الإيمان بأنه لا يعطي ولا يمنع ولا يضر ولا ينفع سواه Na kuhakiki kuthibitisha imani kwamba hakuna yeyote yule anaeweza kutoa na wala anaeweza kuzuia na wala anaeweza kudhuru na wala anaeweza kunufaisha isipokuwa Yeye (yaani: Allah Pekee). ﴾عَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٣ "Na kwa Allah Pekee tawakalini ikiwa nyinyi ni Waumini (wa kwelikweli)." [Al Maaidah 5:23] ﴾فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ ۚ ﴿١٢٣ "basi muabudu Yeye Pekee, na tawakali Kwake ...." [Huud 11:123] Kutawakali ni ibada; haijuzu isipokuwa kwa Mungu. فالتوكل عبادة لا يجوز إلا الله أما التوكيل فيما يقدر عليه المخلوق، كأن توكل أحدا يشتري لك حاجة Ama kuhusiana na kuteua atakaewakilisha katika yale anayoyaweza mahuluku, kama vile kumteua mmoja yeyote yule akununulie kitu. وتوكل أحدا يعمل لك عملا، هذا جائز Na unaweza kumteua mtu wa akuwakilishe kwa (kukufanyia) kazi; hii inajuzu (inaruhusiwa). ﴾فَابْعَثُوا أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمْ هَـٰذِهِ إِلَى الْمَدِينَةِ فَلْيَنظُرْ أَيُّهَا أَزْكَىٰ طَعَامًا فَلْيَأْتِكُم بِرِزْقٍ مِّنْهُ وَلْيَتَلَطَّفْ وَلَا يُشْعِرَنَّ بِكُمْ أَحَدًا ﴿١٩ "Basi tumeni mmoja wenu mjini kwa noti zenu hizi atazame chakula chake kipi kifaacho zaidi kisha akuleteeni chakula hicho; na awe makini na busara, na wala asikutambulisheni kwa mmoja yeyote yule."[Al Kahf 18:19]. Huu (kwenye Aayah) ni uwakilishaji, na uwakilishaji unaruhusiwa هذا توكيل، فالتوكيل جائز Ama kutawakali huwa inamuhusu (yaani:hasa kwa) Allah Pekee أما التوكل فإنه خاصا بالله