NAIBU WAZIRI MILLYA AWATAKA WAFUGAJI KUENDELEZA UFUGAJI BILA WOGA
Ages Media tv
0:00 / 0:00
NAIBU WAZIRI MILLYA AWATAKA WAFUGAJI KUENDELEZA UFUGAJI BILA WOGA
48 просмотров · 4 дня назад
Ages Media tv
295 подписчиков
48 просмотров · 4 дня назад
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Simanjiro, Mhe. James Ole Millya, amewataka wananchi wa Jimbo la Simanjiro kuendelea na shughuli za ufugaji wenye tija, unaolenga kuboresha maisha yao na kuwanufaisha vizazi vijavyo.
Akizungumza na wakazi wa Simanjiro wakati wa ziara yake ya siku mbili jimboni humo, Mhe. Millya amesisitiza umuhimu wa wafugaji kote nchini kuendelea kufanya shughuli za ufugaji kwa kuzingatia maendeleo, akisema Serikali inathamini na kutambua mchango wa sekta ya mifugo katika uchumi wa wananchi na taifa.
Aidha, Mhe. Millya amewahakikishia wafugaji wanaoishi maeneo ya karibu na mapori tengefu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefuta utaratibu wa kukamata mifugo na kuihifadhi hadi kesi inapomalizika.
Kwa mujibu wa Mhe. Millya, utaratibu huo ulikuwa ukiwaathiri wafugaji, akieleza kuwa wakati mifugo inapokamatwa na kuhifadhiwa kwa muda mrefu, baadhi ya wafugaji walipofuatilia mifugo yao baada ya kesi kumalizika walikuta idadi imepungua kutokana na vifo au ukosefu wa matunzo.