Перейти к содержимому

SANDUKU LAKUTWA PORINI LIKIWA LIMEFUNGWA MTWARA KILICHOKUTWA NDANI CHASHANGAZA WENGI

Faida Online TV

0:00 / 0:00

SANDUKU LAKUTWA PORINI LIKIWA LIMEFUNGWA MTWARA KILICHOKUTWA NDANI CHASHANGAZA WENGI

3 984 просмотра · 2 мес. назад
Faida Online TV
24,1 тыс. подписчиков
3 984 просмотра · 2 мес. назад
Mapema hii leo Septemba 01, 2026 Faida Online TV tumepokea taarifa inayohusu kuonekana kwa Sanduku na stuli ndefu Porini katika eneo la Samwange Kitongoji cha Pemba pwani Kijiji cha Naumbu Kusini Mtwara DC, huku Wananchi wakiwa hawajui ndani ya Sanduku hilo Kuna kitu gani. Wananchi hao walikumbwa na wasiwasi baada ya kuona vitu hivyo huku wengine wakihisi kuwa labada ndani ya Sanduku hilo mnaweza kuwa na Pesa au hata vitu vya kishirikina kama nyoka wa kufugwa n.k Ikumbukwe kuwa eneo hilo lipo pembezoni mwa Bahari ya hindi na pia ni mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbiji, hivyo kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa wa Mtwara ililichukulia jambo hilo kwa ukubwa wake na kwenda kulivunja ili kuona kilichopo ndani yake. Baada ya kuvunjwa Sanduku hilo, Kila Mmoja alishangaa maana ndani yake mlikutwa Kipande cha Sanda kinachoonekana kiwekwa muda mrefu, na hakukuwa na kitu kingine chochote.