MAJARIBU NI NINI ? | JE! MAJARIBU YANALETWA NA MUNGU? | UNAWEZAJE KUSHINDA MAJARIBU | TAZAMA
CHARISMA TV
0:00 / 0:00
MAJARIBU NI NINI ? | JE! MAJARIBU YANALETWA NA MUNGU? | UNAWEZAJE KUSHINDA MAJARIBU | TAZAMA
3 088 просмотров · 3 года назад
CHARISMA TV
3,03 тыс. подписчиков
3 088 просмотров · 3 года назад
MAJARIBU NI NINI ? | JE MAJARIBU YANALETWA NA MUNGU? | UNAWEZAJE KUSHINDA MAJARIBU | TAZAMA
Nini maana ya Majaribu?
Majaribu ni ile nguvu ya tamaa mbaya inayokuja na kukutaka ufanye ubaya huo. Ni uovu ambao mwili unataka kufanya alafu pale ambapo roho yako inasimama imara na kusema silifanyi hili maana Mungu yupo pamoja nami na ananiwezesha,hivyo ukashindwa kufanya ule ubaya ambao mwili ulikuwa unataka uufanye. Majaribu yanatokea pale ambapo mwili umehusika kutoa mlango ili yatokee. Maandiko yanasema "roho i radhi lakini mwili ni dhaifu".
Wapo watu wengi sana wanadhania majaribu ni mtaji; sasa kama ni mtaji basi kitu hiki ni cha faida,na itakupasa ukiombee ili kikujilie kwa wingi. Lakini kiuhalisia sio kweli, majaribu sio mtaji kama wengi wanavyodhani.Ukisoma Mathayo 26:41, tunaona Yesu Kristo akiwaonya wanafunzi wake wasiingie majaribuni bali wakeshe wakiomba. Kitu kitakachokufanya usiingie majaribuni ni kukesha na kuomba.Kukesha huku alikomaanisha Yesu Kristo ni ile hali ya roho yako kuwa macho/makini wakati wowote, yaani roho yako kuwa tayari wakati wowote na kujua jambo lolote linalotaka kutokea.
Yakobo 1:12-15, Unapojaribiwa usiseme kuwa unajaribiwa na mtu maana Mungu hamjaribu mtu. Majaribu ni maovu. Wengi wanadhania ile namna ya wao kupitia hali ngumu kama kukosa fedha,kukosa kazi,kuumwa nk, kwamba hayo ni majaribu, lakini sio hivyo. Jaribu lolote ni nguvu iliyo kinyume na Mungu; lakini tumepewa neema ya kuweza Kustahimili/kuyashinda majaribu pale yanapokuja.
1Wakorintho 10:12-13
Lengo la jaribu ni kukuangusha na kukufanya usimtii Mungu bali umtii ibilisi. Anayejidhania kuwa amesimama katika imani basi aangalie asije akatetereka kwa sababu ya jaribu. Majaribu anayoyaleta ibilisi kwa mtu aliyempokea Kristo ni yaleyale ambayo yanayompata yule ambaye hajampokea Kristo. Kwa yule aliyempokea Kristo anayo faida,pale jaribu linapomshinda kwa maana ya kuanguka, ndani ya mtu huyo kunakuwa na nguvu inayomsababishia kukumbuka kuomba rehema na neema za Mungu kwa maana ya kutengeneza na Mungu. Rehema na Neema za Mungu ndio mlango wa kutokea pale ambapo jaribu linapomshinda mtu.
Je unaitaji kujifunza zaidi karibu kanisani Tabata kifuru au wasiliana nasi kupitia namba +255 718 646 364 au +255 682 599 376
#ProphetSimonCharisma #Charismatv #charismageneration #kizazikilichokataakufa #kizazikinachoishimilele #tunaishimpakaunyakuo #uzimanamafanikio
CLICK THE "SUBSCRIBE BUTTON" on the bottom right corner of the video.
Follow Us On:
INSTAGRAM: / prophetsimoncharisma
FACEBOOK: / prophetsimoncharisma
#LCM2023 #UzimanaMafanikio
#charismatv #majaribunimtaji #majaribuninini #majaribu #kuomba #jifunzekuomba #jifunzenenolaMungu #biblianinini #maombiyavita #ombahivikujibiwaharaka #nyimbozakuhabudu #yoteyanawezekana #yesukristo
#gospel #somabiblia #truth #christianity #worship
#believe #holyspirit #spirituality #healing #charismageneration #kizazikilichokataakufa #kizazikinachoishimilele #tunaishimpakaunyakuo #uzimanamafanikio
#scripture #spiritual #grace #loveyourself
#amen #prophetic worship #Haleluya Tv
#prophetic fire #propheticanddeliverance
#propheticandhealingministry
#tanzania #kenya #uganda