Перейти к содержимому

WANAFUNZI MILIONI 1.5 KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA NNE NECTA , YATANGAZA

TANGA MEDIA

0:00 / 0:00

WANAFUNZI MILIONI 1.5 KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA NNE NECTA , YATANGAZA

228 просмотров · 16 часов назад
TANGA MEDIA
28,2 тыс. подписчиков
228 просмотров · 16 часов назад
Wanafunzi 1,591,064 wanatarajiwa kuanza kufanya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la nne , Oktoba 5, hadi Oktoba 6, 2026, huku wavulana wakiwa 764,284, sawa na asilimia 48, na wasichana 826,780, sawa na asilimia 51.9. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Profesa Said Mohamed, upimaji huo ni muhimu katika kubaini kiwango cha wanafunzi katika kumudu stadi mbalimbali za msingi. Amesema upimaji huo huwezesha kujua kiwango cha wanafunzi katika kusoma, kuandika, kutumia lugha ya Kiingereza, kuhesabu na umahiri katika masomo ya lazima, ikiwamo Kiswahili. Wakati huo huo, jumla ya wanafunzi 1,827,367 wamesajiliwa kufanya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili, utakaofanyika Oktoba 7 na 8, 2026. Kati yao, wavulana ni 906,545, sawa na asilimia 49.6, huku wasichana wakiwa 920,822, sawa na asilimia 50.4. Kwa upande wa Kidato cha Pili, wanafunzi 794,713 wameorodheshwa kufanya upimaji mwaka huu, ambapo 786,163 ni wanafunzi wa shule na 8,550 watahiniwa wa kujitegemea. Kati yao, wanafunzi 781,127 watafanya upimaji katika Mkondo wa Jumla, huku 5,036 wakifanya katika Mkondo wa Amali, ambao ulianza kutahiniwa mwaka 2025 kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo. Wanafunzi 1,162 wenye mahitaji maalum wamesajiliwa, wakiwemo wenye uoni hafifu 939, wasioona 78, wenye uziwi 56, ulemavu wa akili 13 na ulemavu wa viungo 76. Upimaji wa Kidato cha Pili utafanyika kuanzia Oktoba 12 hadi 23, 2026.