MTOTO ALIYEPOTEA BADO HAJAONEKANA MTWARA| TUHUMA ZAHAMIA KWA BABA KUMUWEKA KWENYE CHOMBO CHA UVUVI
Faida Online TV
0:00 / 0:00
MTOTO ALIYEPOTEA BADO HAJAONEKANA MTWARA| TUHUMA ZAHAMIA KWA BABA KUMUWEKA KWENYE CHOMBO CHA UVUVI
553 просмотра · 1 мес. назад
Faida Online TV
23,8 тыс. подписчиков
553 просмотра · 1 мес. назад
Siku ya Tarehe 13/06/2026 Faida Online TV (Watu wa Field) tuliripoti habari kuhusu kupotea kwa Mtoto aitwae Bizati Abasi Salumu (10) aliyekuwa akiishi kwenye Kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara mikindani baada ya kutumwa na Bibi yake kwenda kuuza maandazi na tangu hapo hakurudi tena Nyumbani.
Siku ya Tarehe 15/08/2026 tumerudi tena katika Nyumba aliyokuwa akiishi binti huyo kwa ajili ya kufuatilia taarifa hiyo ili kujua kama Familia wamefikia wapi na mpaka sasa matumaini ya kumpata Mtoto huyo aliyekuwa akisoma Darasa la tatu katika Shule ya msingi Naliendele yapoje.
Bibi wa Mtoto huyo ameiambia Faida Online TV kuwa, hapo mwazo Watu walikuwa wakimtuhumu yeye na Bwana wake kuwa ndo wamehusika kumpoteza Mjukuu wao ili Bibi apate mazao mengi Mikoroshoni, na Babu apandishwe Cheo msikitini, ila kwa sasa mambo yamegeuka wanamtuhumu Baba wa Mtoto huyo kuwa amemuweka kwenye chombo cha uvuvi.
Wamezunguka kwa Wataalam wa tiba asili 18 mbao kila mmoja anatoa kauli yake kuhusu mazingira ya Mtoto huyo.
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU