Перейти к содержимому

KUZIFAHAMU KARAMA ZA ROHO NA UTENDAJI WAKE - PART 01 || IBADA YA JUMAPILI | Pst. James Kalekwa

Pastor James Kalekwa

0:00 / 0:00

KUZIFAHAMU KARAMA ZA ROHO NA UTENDAJI WAKE - PART 01 || IBADA YA JUMAPILI | Pst. James Kalekwa

389 просмотров · 1 год назад
Pastor James Kalekwa
2,45 тыс. подписчиков
389 просмотров · 1 год назад
Karama za Ufunuo/Mafunuo B. Neno la hekima Hekima ni utekelezaji wa maarifa na uzoefu uliokusanywa maishani, karama ya neno la hekima hufunua mambo yajayo au yatakayojitokeza siku za usoni. Karama ya Neno la hekima inashughulikia mambo ambayo hayajatokea bado; kwa upande mmoja unafunua makusudi, mipango, shauri la Bwana na Karama ya neno la hekima unajulishwa kwa kuwa mambo yatatokea ili kujiandaa, na kujiweka kwenye nafasi unayopaswa na/au unajulishwa ili yatokee hivyo kuna jambo la kufanya ili yatokee Makusudi ya Mungu ambayo yameshawekwa tayari na hayatatanguka; yanafunuliwa ili mtu ajue kwa lengo la kujiandaa mapema. Neno la maarifa itakakwambia nafasi ambayo imepita au inayoendelea ili ujue nini cha kufanya na hiyo taarifa; lakini neno la hekima inaeleza nini cha kufanya baada ya kupokea taarifa. Mifano ya neno la hekima katika Biblia Mfano #1 1 Wafalme 21:18-19 “Ondoka, ushuke, ukutane na Ahabu mfalme wa Israeli, akaaye katika Samaria; yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ndiko alikoshukia ili alitamalaki. Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.” Taarifa kwenye mstari wa 18, ni neno la maarifa na mstari wa 19 ni neno la hekima kwa kuonyesha nini anafanya na hiyo taarifa. 1 Wafalme 22:34-38 “Mtu mmoja akavuta upinde kwa kubahatisha, akampiga mfalme wa Israeli mahali pa kuungana mavazi yake ya chuma; kwa hiyo akamwambia mwendesha gari lake, Geuza mkono wako, unichukue kutoka katika majeshi; kwa kuwa nimejeruhiwa sana. Pigano likazidi siku ile; mfalme akategemezwa garini mwake, kinyume cha Washami, hata jioni akafa; damu ikatoka katika jeraha yake ndani ya gari. Ikapigwa mbiu jeshini, jua likichwa, kusema, Kila mtu aende mjini kwake, na kila mtu shambani kwake. Hivyo akafa mfalme, akachukuliwa Samaria, wakamzika mfalme huko Samaria. Wakaliosha gari penye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake; (basi ndipo walipooga makahaba); sawasawa na neno la BWANA alilolinena.” Mfano #2: Mtume Yohana na Makanisa saba Ufunuo 2:1-2 “Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;” Mfano #3: Mfalme Yehoshafati 2 Nyakati 20:16-18 “Kesho shukeni juu yao; tazameni, wanakwea kwa kupandia Sisi; nanyi mtawapata penye mwisho wa bonde, mbele ya jangwa la Yerueli. Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa BWANA yu pamoja nanyi. Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za BWANA Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia BWANA.” a. Kupambanua roho Tunapozungumzia Roho tunazungumzia i. Mungu (Uungu) ii. Shetani iii. Mwanadamu iv. Viumbe vya kiroho Kupambanua ni kujua kwa namna ya ndani, kujua kunakowezeshwa na Roho mtakatifu; kwa uwezo au uzoefu wa kawaida mtu hawezi kujua kabisa jambo fulani, Karama zinatenda kazi pale tu ambapo kuna uhitaji. Karama ya Neno la maarifa na neno la hekima ni karama ambazo zinaona katika ulimwengu wa roho ni nini kinaendelea kuhusiana na ulimwengu wa mwili lakini karama ya kupambanua roho ni kwa ajili ya kufahamu nini kinaendelea kwenye ulimwengu wa roho pekee; kujua roho gani iko kazini au roho gani inatenda kazi wakati huo. Kupambanua roho sio kutambua tabia za watu, sio umbea, karama zimeachiliwa kwa ajili ya kujenga sio kubomoa.