Перейти к содержимому

SABABU 4 ZILIZOMFUKUZA NCHIMBI CCM ZAFICHULIWA | KAWAIDA ATOA UNDANI

MJAWIR MEDIA

0:00 / 0:00

SABABU 4 ZILIZOMFUKUZA NCHIMBI CCM ZAFICHULIWA | KAWAIDA ATOA UNDANI

3 780 просмотров · 2 дня назад
MJAWIR MEDIA
14,7 тыс. подписчиков
3 780 просмотров · 2 дня назад
KAWAIDA AELEZA UNDANI SABABU KUFUKUZWA NCHIMBI Asema makosa manne yamepelekea CCM kumfuta uanachama Aeleza alivyofuatwa Dar es Salaam kusikilizwa na akaleta kiburi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) ameeleza undani zaidi wa sababu zilizopelekea Chama cha Mapinduzi kumfuta uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi. Ndugu Kawaida akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika Ofisi za Makao Makuu UVCCM jijini Dodoma leo tarehe 01 Septemba 2026 ambao walitaka kupata undani wa kauli yake aliyoitoa tarehe 29 Agosti 2026 akiwa Ikulu kwenye uapisho wa Makamu wa Rais, Ndugu Deogratius Ndejembi. Ndugu Kawaida ameeleza kuwa Nchimbi aliandikiwa barua kufika Kamati ya Maadili kuhusu makosa manne aliyokutwa nayo na kutakiwa kufika kuhojiwa mkoani Dodoma na Vikao vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu CCM ilibidi vifanyike mkoani humo ila alitoa taarifa ya kuumwa akiwa Dar es Salaam na CCM ikaona ni vyema Wajumbe kwenda Dar es Salaam kwenda kumsikiliza utetezi wake. Aidha, amesema Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM ilisubiri ripoti ya Kamati ya Maadili ambao walisema Dkt. Nchimbi hakutokea kwenye kikao hicho na kuonyesha kiburi kilichopeleka kufukuzwa uanachama. "Kamati ya Maadili ilituletea taarifa kwamba kiongozi huyo alikataa kufika mbele ya Kamati ya Maadili na sisi Wajumbe wa Halmashauri Kuu pamoja na Kamati Kuu tukaadhimia kumfukuza uanachama, nabaki na msimamo wangu thabiti nikisema tumemfukuza uanachama Dkt. Nchimbi sababu ya kiburi chake na kutoheshimu misingi ya Chama chetu," amesema Ndugu Kawaida