TAMASHA LA TATU LA FAHARI YA ZANZIBAR LAFUNGWA RASMI
ZEEA ONLINE TV
0:00 / 0:00
TAMASHA LA TATU LA FAHARI YA ZANZIBAR LAFUNGWA RASMI
6 просмотров · 2 недели назад
ZEEA ONLINE TV
3 подписчика
6 просмотров · 2 недели назад
WAZIRI wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji, Mhe. Shaaban Ali Othman, ameitaka Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) kuyaendeleza mafanikio yaliyopatikana kupitia Tamasha la Fahari ya Zanzibar na kubuni mbinu mpya za kuyahuisha ili kuongeza ufanisi katika siku zijazo.
Amesema tamasha hilo limekuwa jukwaa muhimu kwa wananchi, hususan wajasiriamali, kupata fursa mbalimbali za kiuchumi, hivyo ZEEA inapaswa kuhakikisha fursa hizo zinaendelea kuwa na manufaa kwa wananchi.
Akifunga Tamasha la Tatu la Fahari ya Zanzibar 2026, Mhe. Shaaban ameitaka ZEEA kuhakikisha biashara za wajasiriamali zinarasimishwa, kupatiwa elimu ya biashara na kutafutiwa masoko ya bidhaa zao sambamba na kuwaunganisha na mitandao ya wafanyabiashara wakubwa ili wapate fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA), Juma Burhan Mohamed, amesema Tamasha la Fahari ya Zanzibar limethibitisha kwa vitendo kauli ya “Bidhaa Zetu, Fahari Yetu”, kwa kuwa limewapa wajasiriamali fursa ya kuonesha na kutangaza bidhaa zao, kukutana na wateja, kubadilishana uzoefu na wafanyabiashara wengine, pamoja na kufungua fursa mpya za masoko na kukuza biashara zao.
Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Fredy Liundi, amesema Mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na ZEEA katika kujenga mazingira bora kwa wafanyabiashara, kupitia utoaji wa elimu ya biashara, kukuza biashara zao na kuwaunganisha na masoko ndani na nje ya Zanzibar.