Перейти к содержимому

WAZIRI AAGIZA UKARABATI WA KITUO CHA KUFUA UMEME HALE UKAMILIKE JULAI 31, 2026

Tanga Tanzania TV

0:00 / 0:00

WAZIRI AAGIZA UKARABATI WA KITUO CHA KUFUA UMEME HALE UKAMILIKE JULAI 31, 2026

133 просмотра · 2 месяца назад
Tanga Tanzania TV
25,4 тыс. подписчиков
133 просмотра · 2 месяца назад
Serikali haitaongeza muda wa mradi; itachukua hatua za kimkataba kwa Mkandarasi. Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius J. Ndejembi amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ukarabati wa Kituo cha Kufua Umeme Hale kukamilisha kazi ifikapo tarehe 31 Julai 2026, akieleza kuwa Serikali haitaongeza muda wa ziada iwapo atashindwa kukamilisha kazi hiyo kwa wakati. Ametoa agizo hilo tarehe 29 Juni 2026 wakati akikagua maendeleo ya ukarabati mkubwa wa Kituo cha Kufua Umeme Hale kilichopo mkoani Tanga katika Bonde la Mto Pangani kilichozinduliwa mwaka 1964. Ukarabati huo unalenga kurejesha ufanisi wa kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha megawati 21. #tanga_tanzania