Перейти к содержимому

WAZIRI AINGILIA KATI SAKATA LA BAJAJI MBEYA, AAGIZA UONGOZI USIMAMISHWE

Mwananchi Digital

0:00 / 0:00

WAZIRI AINGILIA KATI SAKATA LA BAJAJI MBEYA, AAGIZA UONGOZI USIMAMISHWE

4 108 просмотров · 6 часов назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
4 108 просмотров · 6 часов назад
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Profesa Riziki Shemdoe ameondoa zuio la kutoingia kwa bajaji katika barabara kuu ya Tanzam jijini Mbeya. Hatua hiyo inaambatana na maelekezo mahususi aliyompa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini. Akizungumza leo Oktoba 22, 2026 wakati wa ziara yake jijini humo, Profesa Shemdoe amemwelekeza Mkuu wa Mkoa kusitisha usajili wa bajaji mpya. Aidha, ameagiza kuundwa kwa timu maalumu itakayochunguza mazingira ya vyombo vya moto, ikiwemo upangaji wa ruti. Waziri amebainisha kuwa idadi ya sasa ya bajaji 6,000 inatosha, wakati tathmini ya miundombinu ikiendelea. Vilevile, amemtaka Mkuu wa Mkoa kufuatilia malalamiko dhidi ya uongozi uliopo madakarani wa Umoja wa Bajaji, ambao unakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na mali. Profesa Shemdoe ameagiza uongozi huo usimamishwe na badala yake uundwe uongozi wa muda wa mpito.