Перейти к содержимому

Hii hapa Homilia Nzima ya Padre Mkwizu Iliyozua Mjadala Mtandaoni/Akemea Matumizi mabaya ya Madaraka

Breez Online Tv

0:00 / 0:00

Hii hapa Homilia Nzima ya Padre Mkwizu Iliyozua Mjadala Mtandaoni/Akemea Matumizi mabaya ya Madaraka

2 066 просмотров · 9 ч назад
Breez Online Tv
93,5 тыс. подписчиков
2 066 просмотров · 9 ч назад
PADRE JONATHAN MKWIZU AONYA DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA, ASEMA WENYE NGUVU WAMEWAUMIZA WENGI Katibu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Padre Jonathan Mkwizu, ametoa onyo kali dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka, akisema baadhi ya watu wenye vyeo na nguvu wamekuwa chanzo cha mateso kwa wengine, wakiwemo wajane na watoto yatima waliopoteza wapendwa wao kutokana na maamuzi ya watu wenye mamlaka. Padre Mkwizu ameyasema hayo wakati wa homilia katika Misa Takatifu ya Dominika ya 30 ya Mwaka A wa Kanisa, iliyoadhimishwa katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki la Same, akisisitiza kuwa cheo, ulinzi na nguvu alizonazo mtu havimpi haki ya kuwatesa, kuwateka au kutoa amri za kuangamiza maisha ya wengine. Akifafanua ujumbe wa masomo ya siku hiyo, Padre Mkwizu amesema kuna watu wanaotumia mamlaka yao kufanya chochote wanachotaka kwa sababu wana nguvu na ulinzi, huku wakisahau kuwa matendo yao yanaweza kuwa sababu ya watu wengine kulia, kupoteza wenza wao na hata kuishi bila wazazi. “Ni watu wangapi leo wanalia? Pengine ni wajane kwa ukweli wajane kabisa, kwa sababu wewe umekuwa sababu ya ujane wao. Ni wangapi ambao leo pengine wamepoteza wazazi wao kwa sababu ya amri yako wewe mwenye nguvu?” amehoji Padre Mkwizu. Amesema Neno la Mungu katika Kitabu cha Kutoka linatoa onyo kali kwa wale wanaowatesa wageni, wajane na watoto yatima, likisisitiza kuwa Mungu husikia kilio chao na hasira yake huwaka dhidi ya wanaowadhulumu. Padre Mkwizu amesisitiza kuwa onyo hilo halikuhusu Waisraeli pekee, bali linawahusu pia watu wa kizazi cha sasa, akiwataka kujichunguza na kuacha kutumia vyeo, mafanikio na nguvu zao kuwaumiza wengine. Amesema kila mtu anapaswa kujitambua kuwa anamtegemea Mungu, hata anapokuwa na mafanikio, cheo au uwezo mkubwa, kwa sababu kuna wakati katika maisha kila mmoja amewahi kuwa mhitaji na kutegemea msaada wa wengine. Aidha, amewataka watu waliofanikiwa kutosahau walikotoka, akitumia mfano wa Misri kuonyesha hali ya mateso ambayo mtu anaweza kuwa amepitia kabla ya kupata uhuru na maisha bora. “Usisahau Misri yako ukamrudisha mwenzako katika Misri ile ambayo yeye ameipita. Misri ya mtu inaweza ikawa ni mateso makubwa. Usiwe wa kwanza kumpeleka mwenzako Misri baada ya kutoka Misri,” amesisitiza. Ameeleza kuwa Misri ya mtu inaweza kuwa hali ya kukosa mtu wa kumtegemea, kama vile mume kwa mjane au wazazi kwa mtoto yatima, hivyo kuwataka wenye uwezo kutowarudisha wengine katika mateso waliyokwisha kuyapitia. Katika hatua nyingine, Padre Mkwizu ametoa wito wa kutubu na kuomba msamaha kwa Mungu kwa makosa yaliyofanywa kupitia mamlaka, vyeo na nguvu walizo nazo watu, hasa pale ambapo uwezo huo umetumika kuwaumiza wengine. Imeandikwa na Izahaki Mwacha Video Source: Radio Maria Tanzania #KanisaKatoliki #Tanzania #BaloziwaAmani #breezonlinetv #woisooriginalproducts #mkombozicommercialbank #news