RC Kheri James Afika Site Kukagua Mitambo iliyofungwa Machinjio ya Kisasa Ngelewala Iringa Manispaa
Focus TV Tanzania
0:00 / 0:00
RC Kheri James Afika Site Kukagua Mitambo iliyofungwa Machinjio ya Kisasa Ngelewala Iringa Manispaa
3 715 просмотров · 3 нед. назад
Focus TV Tanzania
79,7 тыс. подписчиков
3 715 просмотров · 3 нед. назад
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa machinjio ya kisasa ya Ngelewala, iliyopo katika Kata ya Mwang'ata, Manispaa ya Iringa, uwekezaji mkubwa uliogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya ufungaji wa mitambo ya kisasa ya uchinjaji wa ng'ombe na mbuzi.
Ziara hiyo iliyofanyika Septemba 24,2026, imelenga kujiridhisha na hatua iliyofikiwa katika ufungaji wa mitambo hiyo ambayo inaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mifugo na biashara ya nyama mkoani Iringa.
Mradi huu ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi wa Manispaa ya Iringa na Mkoa kwa ujumla, kwani ulianzishwa tangu mwaka 2008 lakini ulikuwa ukisuasua kwa miaka mingi. Hata hivyo, mapinduzi makubwa na ya kihistoria yameonekana wazi mwaka 2026 kufuatia jitihada za makusudi zilizowekwa na serikali kukamilisha miundombinu na ufungaji wa mitambo hiyo ya kisasa.
Ziara hii ya RC Kheri James inajenga imani kubwa kwa wananchi kwamba miradi ya kimkakati iliyokwama kwa muda mrefu sasa inakamilishwa kwa kasi na ufanisi wa hali ya juu ili kuleta maendeleo endelevu.
Focus TV ni chombo cha habari cha mtandaoni kinachorusha Maudhui yanayohusu Habari, Mitindo ya Maisha, Utamaduni, Michezo na Burudani kwa kuyaongezea thamani kwa maslahi ya umma.
.................
Focus TV is one of the Best Online TV Conveying Content and adding values for the public interest.
Focus TV is here to provide you with contents covering News, Education, Lifestyles, Culture, Sports and Entertainments.
Focus TV imesalijiliwa Nchini Tanzania na kupewa Leseni ya kurusha maudhui mitandaoni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Asante kwa kuchagua kutufuatilia | Thanks for Subscribing
We Love You | Tunakupenda
Regards
Team Focus TV Tanzania
#FocusTVTanzania