SEHEMU YA 1: MIAKA 32 YA HUDUMA! SIMULIZI YA MCHUNGAJI ALIYETEMBEA KWA MIGUU KUHUBIRI INJILI
Mazingira Fm
0:00 / 0:00
SEHEMU YA 1: MIAKA 32 YA HUDUMA! SIMULIZI YA MCHUNGAJI ALIYETEMBEA KWA MIGUU KUHUBIRI INJILI
123 просмотра · 5 мес. назад
Mazingira Fm
2,77 тыс. подписчиков
123 просмотра · 5 мес. назад
Mwaka 1994, mtumishi wa Mungu Amos Festo alianza safari ya wito wa kichungaji.
Si katika mazingira ya kifahari, wala si kwa urahisi wa usafiri na maisha ya starehe.
Bali alianza katika kijiji kilichokuwa umbali wa zaidi ya kilometa 50 kutoka Tarime mjini.
Safari ngumu, njia za vumbi, milima na mabonde… lakini moyo wake ulikuwa na moto wa kuhubiri Injili ya Kristo.
Baadaye akahamishwa tena kwenda kituo kingine, kilometa 12 kutoka Tarime mjini…
Na bado hakuchoka.
Miguu yake ikawa usafiri wa Injili.
Ametembea kwa miguu kwa miaka mingi kwenda kuhubiri, kuwafariji waliovunjika moyo, kuwaombea wagonjwa, na kusimama pamoja na waumini wake katika nyakati zote.
Kwa miaka 32 ya huduma, ameona mengi…
Ameshuhudia machozi yakigeuka furaha…
Wagonjwa wakipokea uponyaji…
Waliokata tamaa wakipata tumaini…
Familia zikirejea kwa Mungu…
Na maisha ya watu wengi yakibadilishwa kupitia huduma yake.