Ijue elimu kuhusu Simba na namna ya kujihami | UTV Tanzania
UTV Tanzania
0:00 / 0:00
Ijue elimu kuhusu Simba na namna ya kujihami | UTV Tanzania
11 238 просмотров · 2 недели назад
UTV Tanzania
180 тыс. подписчиков
11 238 просмотров · 2 недели назад
Msomi na Mtafiti wa Simba, Monte Kalyahe, amesema simba ni wanyama wanaoishi kwa makundi na hulinda maeneo yao, yanayojulikana kama himaya. Amesema licha ya simba kuwa wanyama wakubwa walao nyama, si kila wakati huwa tishio kwa binadamu, kwani tabia zao hutegemea mazingira na namna wanavyokutana na watu.
Dkt. Kalyahe anaeleza kuwa simba hutumia harufu, ikiwemo alama za mkojo na majimaji mengine ya mwili, pamoja na sauti na alama za mikwaruzo, kuwasiliana na kutambua mipaka ya himaya zao. Simba wanapopita katika maeneo yao huacha alama hizo ili kuashiria uwepo wao na kuwajulisha simba wengine kuhusu umiliki wa eneo hilo.