NSSF TABORA IMETOA MSAADA WA VIFAA SAIDIZI KWA WATOTO WENYE UTINDIO WA UBONGO HOSPITALI YA KITETE
KITETE REGIONAL REFERRAL HOSPITAL (KITETE RRH TV)
0:00 / 0:00
NSSF TABORA IMETOA MSAADA WA VIFAA SAIDIZI KWA WATOTO WENYE UTINDIO WA UBONGO HOSPITALI YA KITETE
159 просмотров · 7 дней назад
KITETE REGIONAL REFERRAL HOSPITAL (KITETE RRH TV)
348 подписчиков
159 просмотров · 7 дней назад
#trending #afya #africa #amniga #imani #wizarayaafya #motivation #aflao #live #news #nssf #charity #hope
NSSF TABORA YATOA VIFAA SAIDIZI KWA WATOTO WENYE UTINDIO WA UBONGO HOSPITALI YA KITETE*
TABORA
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tabora limetoa vifaa saidizi kwa watoto wenye changamoto ya utindio wa ubongo wanaopatiwa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kitete, Dkt. Swaumu Kimaro, ameishukuru NSSF kwa msaada huo, akieleza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuboresha mazingira ya huduma kwa watoto hao.
“Tunawashukuru NSSF kwa kutambua mahitaji ya watoto wenye changamoto ya utindio wa ubongo na kuchukua hatua ya kuwasaidia. Vifaa hivi vinaongeza faraja, usalama na uwezo wa watoto kupata huduma stahiki. Tunaamini ushirikiano huu utaendelea kuleta matokeo chanya kwa watoto na familia zao.”
Kwa upande wake, Afisa Utawala wa NSSF Mkoa wa Tabora, Sosten Mtena, amesema msaada huo umetolewa kwa lengo la kuunga mkono jamii na juhudi za Serikali katika kuboresha huduma na ustawi wa wananchi.
“NSSF inaamini kuwa jukumu letu siyo tu kutoa huduma za hifadhi ya jamii, bali pia kushiriki katika shughuli zenye matokeo chanya kwa jamii. Msaada huu ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali na Hospitali ya Kitete katika kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanapata mazingira bora ya huduma na ustawi.”
Msaada huo ni sehemu ya jitihada za NSSF za kushirikiana na jamii katika kuboresha ustawi wa makundi yenye mahitaji maalum, huku ukiunga mkono juhudi za Hospitali ya Kitete katika kutoa huduma zenye utu, usalama na ubora.
Hospitali ya Kitete unaendelea kuwakaribisha wadau kushirikiana katika kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii, ikiwa na msisitizo katika huduma bora, salama, zenye utu na zinazomweka
Afya yako ni kipaumbele chetu karibu tukuhudumie
Heri ya wiki ya huduma kwa wateja