Haya Maumbile Yangu - Fatma Issa #zanzibartaarab #pwani #oldisgoldsongs #zamanı
Zanzibar orchestra
0:00 / 0:00
Haya Maumbile Yangu - Fatma Issa #zanzibartaarab #pwani #oldisgoldsongs #zamanı
33 595 просмотров · 10 месяцев назад
Zanzibar orchestra
11,3 тыс. подписчиков
33 595 просмотров · 10 месяцев назад
HAYA MAUMBILE YANGU
Ubinafsi na choyo , nyoyoni vya wasumbua
Kutwa kazi yenu hiyo , zimewajawa shakawa
Kwangu yepi muonayo , mageni msoyajua
Kufanya niyapendayo , kwangu kosa limekuwa
Aaaaah Aaaaah Aaaaah Aaaaah Aaaaah
Hilo haliwezekani hili haliwezekani
Na wala halitokuwa
Leo nakuelezeni muache kunichungua
Msijitie shidani haya nimejaaliwa
Kwani hasa jambo gani , mie la kulaumiwa
Kama baya kwenu nyie , kwangu nnaona sawa
Nawambia msikie , msiofahamikiwa
Fedhehani msingie , kukaa kujizuzua
Lilobaki mnachie , sitaki kudhulumiwa
Wengi wamenihasimu wapo walonihasimu
Na thamani kunitoa
Mwapita kumwaga sumu ni laumu kutupiwa
Nami ni mwanaadamu si vyema kunibagua
Nami ni mja mwenzenu hata mkinichukia
Aibu yangu ndo yenu kama mtafikiria