Перейти к содержимому

WAZAZI WAFURAHISHWA NA KUANZA KUTUMIKA KWA SHULE SHIKIZI YA ULEDI TABORA

Cg Online Tv

0:00 / 0:00

WAZAZI WAFURAHISHWA NA KUANZA KUTUMIKA KWA SHULE SHIKIZI YA ULEDI TABORA

70 просмотров · 1 день назад
Cg Online Tv
97,6 тыс. подписчиков
70 просмотров · 1 день назад
#CgOnlineTv #Tabora Wazazi katika Mtaa wa Uledi, Kata ya Mpera, Manispaa ya Tabora, wameeleza kufurahishwa na kuanza kutumika kwa Shule Shikizi ya Uledi, wakisema hatua hiyo imewapunguzia watoto wao changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata elimu katika shule mama ya Majengo. Wakizungumza na CG FM Radio, wazazi hao wamesema kuanza kutumika kwa shule hiyo kutawasaidia watoto kupata elimu karibu na makazi yao, huku wakieleza kuwa uwepo wa shule hiyo ni suluhisho la changamoto ya umbali iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa eneo hilo. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Uledi, John Mwanda, ameiomba Serikali kwa kushirikiana na wananchi kuendeleza juhudi za kukamilisha miundombinu muhimu iliyosalia, ili shule hiyo iweze kutimiza vigezo vinavyotakiwa na mamlaka husika kwa ajili ya kupata hadhi ya shule ya msingi kamili. Mwanda amesema ushirikiano kati ya Serikali na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha ujenzi wa miundombinu hiyo unakamilika, hatua itakayosaidia kuongeza uwezo wa shule kutoa huduma za elimu kwa watoto wengi zaidi katika eneo hilo. Shule Shikizi ya Uledi imeanzishwa kwa juhudi za wananchi kwa kushirikiana na Serikali ili kupunguza changamoto ya umbali kwa watoto waliokuwa wakisoma katika Shule ya Msingi Majengo, iliyopo Kata ya Mpera, Manispaa ya Tabora.