KWAMROMBO SDA CHOIR - ARUSHA TZ || UTUME || OFFICIAL
KWAMROMBO SDA CHOIR
0:00 / 0:00
KWAMROMBO SDA CHOIR - ARUSHA TZ || UTUME || OFFICIAL
2 283 просмотра · 4 дня назад
KWAMROMBO SDA CHOIR
570 подписчиков
2 283 просмотра · 4 дня назад
🎶 *UTUME | SAUTI MOJA, UTUME KWA WOTE* 🎶
Tunasherehekea miaka 2,000 ya utume tangu Yesu Kristo abatizwe na kuanza huduma Yake ya kuhubiri Injili. Tangu wakati huo, ujumbe wa wokovu umeendelea kuhubiriwa kupitia mitume, wafia dini, wanamatengenezo, na waumini wa vizazi mbalimbali. Leo, jukumu hilo linaendelea kuwa letu. "Utume lazima uwe wa kwanza!"
🌍 Ulimwengu wetu ni uwanja wa utume! Popote ulipo, kuna nafasi ya kumtumikia Mungu na kuwafikia wengine kwa Habari Njema za Yesu Kristo. Mungu hatumi wavunaji mahali pasipo na mavuno. Hivyo basi, tusisubiri kwenda mbali ili kutimiza utume; tuanze pale tulipo, tukitumia vipawa na fursa tulizopewa na Mungu.
Kupitia wimbo huu, tunahamasishana kusimama pamoja katika kuhubiri Injili, kuleta watu kwa Kristo, na kuendeleza utume wa Kanisa. Kila mshiriki ana nafasi, kila sauti ina umuhimu, na kila mmoja anaitwa kuwa sehemu ya mavuno ya Bwana.
Kwaya inaungana na kauli mbiu ya Kanisa la Waadventista Wasabato: “OneVoice Mission for All” — “Sauti Moja, Utume kwa Wote.” Tukiwa na moyo mmoja na kusudi moja, tuinue sauti zetu kumtangaza Yesu Kristo na kuuharakisha utume Wake.
📣 Ujumbe wetu ni mmoja: SAUTI MOJA, UTUME KWA WOTE!
🙏 Barikiwa unaposikiliza wimbo huu. Mungu akutie moyo kuwa mtume wa Injili popote ulipo, na maisha yako yawe ushuhuda wa upendo na wokovu unaopatikana ndani ya Yesu Kristo.
#Utume #SautiMojaUtumeKwaWote #OneVoiceMissionForAll #SDA #WaadventistaWasabato #Injili #UtumeWaKanisa #YesuKristo #KwayaYaWaadventista