SERIKALI YAINGILIA KATI KUWAOKOA WATOTO 4 WADOGO WANAOISHI BILA WAZAZI, WAWILI WAMEACHA SHULE
Mwananchi Digital
0:00 / 0:00
SERIKALI YAINGILIA KATI KUWAOKOA WATOTO 4 WADOGO WANAOISHI BILA WAZAZI, WAWILI WAMEACHA SHULE
5 627 просмотров · 1 мес. назад
Mwananchi Digital
1,22 млн подписчиков
5 627 просмотров · 1 мес. назад
Taasisi za Serikali mkoani Kilimanjaro, zimeingilia kati na kuwaondoa watoto wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 11, katika nyumba ambayo waliachwa na wazazi wao tangu mwezi Aprili mwaka huu, na wazazi hao kwenda shughuli za Kilimo huko Simanjiro mkoani Manyara.
Watoto hao walikutwa Ijumaa ya Agosti 14, 2026 katika mtaa wa Relini kata ya Bomambuzi Manispaa ya Moshi, wakiishi katika mazingira magumu ikiwamo kuomba msaada wa chakula kutoka kwa majirani wema huku watoto wawili wanaosoma darasa la tatu wakiwa wameacha shule.
Taasisi hizo zikihusisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mkoa wa Kilimanjaro, Ofisi ya Ustawi wa Jamii mkoa wa Kilimanjaro, Dawati la Jinsia mkoa Kilimanjaro, Polisi Kata, Ofisa Mtendaji mtaa wa Relini na mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo, Elizabeth Mpute, zilichukua uamuzi mzito wa kuwaondoa watoto hao na kuwapeleka eneo salama.