KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING [ 23 SEPTEMBER 2026
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
0:00 / 0:00
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING [ 23 SEPTEMBER 2026
3 699 просмотров · Трансляция закончилась 5 часов назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
64,7 тыс. подписчиков
3 699 просмотров · Трансляция закончилась 5 часов назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING [ 23 SEPTEMBER 2026
UJUMBE WA LEO : WAKUU WALIOFUNGWA
NENO KUU:
Isaya 22 : 3
Wakuu wako wote wamekimbia pamoja, Wamefungwa wasiutumie upinde. Wote walioonekana wamefungwa pamoja, Wamekimbia mbali sana.
2. Wanashindwa kuwa na uhuru wa kutumia mamlaka ya ukuu wao katika mambo ya msingi.
2 Samweli 3:6-11
6 Ikawa, wakati vilipokuwapo vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi, Abneri akajipatia nguvu nyumbani kwa Sauli.
7 Basi Sauli alikuwa na suria, jina lake akiitwa Rispa, binti Aya; Ishboshethi akamwuliza Abneri, Kwa nini umeingia kwa suria ya babangu?
8 Basi Abneri akakasirika kwa maneno ya Ishboshethi, akasema, Je! Mimi ni kichwa cha mbwa, aliye wa Yuda? Hata leo hivi nawafanyia fadhili nyumba ya Sauli babako, na ndugu zake, na rafiki zake, nisikutie wewe mkononi mwa Daudi; nawe hata hivyo wanitia hatiani leo kwa mwanamke huyu.
9 Mungu amfanyie Abneri vivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile Bwana alivyomwapia;
10 kuupitisha ufalme toka nyumba ya Sauli, na kukisimamisha kiti cha Daudi juu ya Israeli, na juu ya Yuda, toka Dani mpaka Beer-sheba.
11 Wala hakuweza kumjibu Abneri tena, kwa sababu alimwogopa.
3. Kuishi maisha ya kiwango cha chini kuliko ukuu wake, ama maisha tofauti na ilivyopaswa.
Waamuzi 6:11-12
11 Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
12 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa.
Waamuzi 16:21
21 Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
MAMBO YANAYOSABABISHA WAKUU KUFUNGWA
1. Sonona (Msongo wa mawazo) ~ Depression
Wakuu wamewekwa kwa ajili ya mambo makubwa na kushughurika changamoto ngumu.
Kutoka 18:21-22, 26
21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;
22 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.
26 Nao wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno dogo wakaliamua wenyewe.
Inatazamiwa kwamba Mtu atakuwa na majibu ya changamoto ngumu zilizopo.
1 Samweli 30:3-6
3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka.
4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena.
5 Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli.
6 Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake.
Inapotokea mtu mkuu ameshindwa kuleta suluhisho ya changamoto ngumu inayomkabili, anaweza kujikuta kwenye kifungo cha msongo wa mawazo, na kukwama pamoja na uwezo alionao.
1 Wafalme 19:9-10
9 Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya?
10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.
2. Mtazamo.
Waamuzi 8:20-21
20 Kisha akamwambia Yetheri mwanawe mzaliwa wa kwanza, Haya, simama, uwaue hawa. Lakini huyo kijana hakutoa upanga wake; maana, akacha, kwa sababu alikuwa ni kijana tu.
21 Ndipo hapo Zeba na Salmuna wakasema, Simama wewe ukatuangukie sisi; kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Basi Gideoni akasimama, akawaua Zeba na Salmuna, akazitwaa koja zilizokuwa katika shingo za ngamia zao.
Muhubiri :Mwalimu, George Mwakabago
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com