HWTZ KUJENGA KONGANI YA VIWANDA 150 BAGAMOYO
Uwekezaji TV
0:00 / 0:00
HWTZ KUJENGA KONGANI YA VIWANDA 150 BAGAMOYO
2 397 просмотров · 2 недели назад
Uwekezaji TV
2,41 тыс. подписчиков
2 397 просмотров · 2 недели назад
Karibu katika fursa nyingine kubwa ya uwekezaji. Hapa ni Eneo Maalum la Kiuchumi Bagamoyo, chini ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania – TISEZA, lenye takribani hekta 9,800 zilizotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uwekezaji. Eneo hili sasa linazidi kubeba sura mpya ya Tanzania ya viwanda, likivutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Miongoni mwa wawekezaji ni kampuni ya HWTZ kutoka China, inayotekeleza mpango wa kujenga kongani ya viwanda itakayojumuisha zaidi ya viwanda 150.
Mkurugenzi wa Bagamoyo SEZ Felix Michael anaeleza kuwa kampuni hii ni moja kati ya wawekezaji makubwa ya uzalishaji wa viwanda 500 kutoka nchini China wapo Bagamoyo wakiwa wamekabidhiwa hekta 500 kwa ajili ya utekelezaji wa kongani hiyo kubwa kuliko zote barani Afrika ambayo inatarajiwa kujumuisha viwanda zaidi ya 150 huku ikizalisha ajira zaidi ya 5,000.
Mradi huo utakapokamilika, ukiwa na viwanda vya kuunganisha magari madogo na makubwa, pamoja na kiwanda cha bidhaa za chuma kitakachozalisha coil, nondo na bidhaa za galvanized iron. Hii ina maana ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa ndani ya nchi, kupanua fursa za ajira na kutoa nafasi kwa Watanzania kupata ujuzi na teknolojia katika sekta ya viwanda.
Kwa TISEZA, uwekezaji huu ni zaidi ya kujenga viwanda. Ni sehemu ya jitihada za kujenga uchumi unaotegemea uzalishaji, kuongeza ajira na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi. Kupitia kurahisisha usajili wa miradi, vibali na huduma mbalimbali za uwekezaji, TISEZA inalenga kupunguza urasimu na kuweka mazingira yanayomwezesha mwekezaji kuanzisha na kukuza biashara kwa ufanisi.
Na nyuma ya hatua hizi kuna mwelekeo mpana wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambao umeweka msisitizo katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, kuvutia mitaji na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi. Kuanzishwa kwa TISEZA na msukumo wa kurahisisha huduma kwa wawekezaji ni sehemu ya mwelekeo huo. Bagamoyo sasa si eneo la uwekezaji pekee, bali ni taswira ya Tanzania inayojenga mazingira bora kwa mitaji, viwanda, ajira na uchumi unaozalisha ndani ya nchi.