TPHPA YATOA RUZUKU YA "NEMO" KUDHIBITI WADUDU KWENYE PARACHICHI.
NJOMBE TC
0:00 / 0:00
TPHPA YATOA RUZUKU YA "NEMO" KUDHIBITI WADUDU KWENYE PARACHICHI.
45 просмотров · 3 нед. назад
NJOMBE TC
670 подписчиков
45 просмотров · 3 нед. назад
Agosti 28, 2026 Serikali kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imetoa ruzuku ya kiuatilifu hai aina ya NEMO kwa wakulima wa parachichi katika Halmashauri ya Mji Njombe, hatua inayolenga kudhibiti wadudu waharibifu, hususan False Codling Moth (FCM) ili kulinda ubora wa mazao na kuongeza ushindani wa parachichi za Tanzania katika masoko ya kimataifa.
Katika hatua hiyo, TPHPA imetoa ruzuku ya kiuatilifu hai aina ya NEMO kwa zaidi ya wakulima 50 katika Kata ya Kifanya na Yakobi, ambao mashamba yao yatatumika kama mashamba darasa kwa ajili ya kuonesha ufanisi wake katika kudhibiti wadudu waharibifu wa parachichi.