Kaa La Moto - Barua kwenda Dar es Salaam
KAA LA MOTO
0:00 / 0:00
Kaa La Moto - Barua kwenda Dar es Salaam
16 132 просмотра · 5 дней назад
KAA LA MOTO
56,7 тыс. подписчиков
16 132 просмотра · 5 дней назад
East Africa Hip Hop Artist, Songwriter, and Cultural practitioner Kaa La Moto, Performing a record 'Barua kwenda Dar es Salaam, Off the E,P "Ndugu wa Mbali" Side B
Written by Kaa La Moto
Music produced by Sango
Stream Ndugu wa mbali E.P now
https://dizastavina.com/ndugu-wa-mbali/
Barua kwenda Dar es Salaam lyrics..
Hi nesi nesi tafadhali basi , nipe hata nafasi tu nijibu...niongee...
Story ya kwako, mkosa mimi sawa.
Story ya kwako, mkosa mimi aah.
Hata nikikwambia jombaa, huwezi amini.
Akili ziliniruka, nilipotoka mahakamani.
Nilikosa amani,
Mwili wote uliweweseka, majibu sikudhani.
Kwamba rafiki yangu kipenzi, yuko kizimbani.
Na leo narudi nyumbani, namuacha gerezani.
Aah..
Bado nakumbuka, dili zote za madini.
Zile za marasini, mpaka za mererani.
Skunka theluji, na zigi ya afrika kusini.
Mguu ya kuku mbuchi, na nduchi za magarini.
We ni mwana unajua, siwezi nikasahau mishe.
Niliporudi nilikausha, ili afande zipite.
Kitaa walifanya msako, kidogo tu wanishike.
Watafute rafiki yako yeyote, wamkamate.
Hapo ndio nikajitia uchizi, na kujirukisha akili.
Waliniseka potrizi, na mahospitali mbali mbali.
Aisee nilikula hadi madawa, kupotezee tu ramani.
Huwezi dhani ingekua rahisi tu, kuishi uraiani.
Mara nakua sawa, napagawa hayawani.
Nilizirudisha kidogo, najikupa mabatani.
Ili mradi wasinisome, mtu wa pombe na majani.
Ila sikua na furaha, na sikujua namna gani.
Nawezaje kukutembea, kujua na hali.
Ujumbe ulinitumia, haki siwezi jibu maswali.
Kuhusu mke na watoto wako, hapo nakubali.
Ila kufika kwako ilikua ngumu, waliweka ma askari.
Na wala sio kweli, eti mi nimekua naponda mali.
Mgao wako mpo, kuhusu hilo wala usijali.
Hawawezi trace kitu, nimezisunda mbali.
Nitakwambia kila kitu, mimi nikikuona afadhali.
Sema nimekua mteja, na mwanzo nilianza na ndumu
Nachanganya vitu vingi, dokta alisemea ni sumu.
Na yote ni kwasababu, najua unapitia magumu.
Na msongo wa mawazo, toka walipotoa hukumu.
Mchana niko freretown, usiku maeneo.
Hadi natelekeza familia, kisa ni kileo.
Angekueko, rafiki wa kweli nisingewaza.
Pia mimi napitia, usione nimenyamaza.
Sema najikaza kiume, wasinisome.
Familia ikigonjeka waumwe, hadi wapome.
Karo ikisumbua niliamua, pia wasisome.
Yote nikisubiri lini utarudi, ili watukome.
Na siwezi kusahau, hata dunia ingekua danga.
Mara zote tuliharibu Dar, tunavukia Namanga.
Uwizi wa karafuu, Zanzibar na Tanga.
Nakumbuka tukizoza, sana mjini sana shamba..
Uskaji, ulikufanya ukajitoa muhanga.
Haiwezi kutokea, nikakuekea X ka wakanda.
Kanda ya ziwa kaskazini, kusini na vanga.
Dili harama tukipitisha, shimoni kijanja.
Umebeba msalaba, ambao sote mbao zinahusu.
Ndugu ni ndugu, ukinishikia kisu inageuka butu.
Usione sifikirii, sikupenda we kua maabusu.
Nimehangaika sana na wakili, huku na huku
I live by the code, halafu wagumu tunakaza.
Sema imekua vigumu, toka nimekupoteza braza.
Sometimes hua nawaza, upendo wako zaidi ya ndugu
Kwa lile tundu la lissu, anaweza kuliziba sugu.
Ni mwaka sasa, wamenipeleka,reharb Mewa.
Familia inahoji, kama nimepoteza ngekewa.
Walikata mawasiliano, ndio maana nilichelewa.
Ilinibidi nimhonge nesi, ndio nafasi nikapewa.
Am sorry for the late reply D,
Kaa La Moto.....