Kaa La Moto - KIPCHOGE
KAA LA MOTO
0:00 / 0:00
Kaa La Moto - KIPCHOGE
13 903 просмотра · 3 недели назад
KAA LA MOTO
56,7 тыс. подписчиков
13 903 просмотра · 3 недели назад
East Africa Hip Hop Artist, Songwriter, and Cultural practitioner Kaa La Moto, Performing a record 'KIPCHOGE, Off the E,P "Ndugu wa Mbali" Side B
Written by Kaa La Moto
Music by Masta Kip & Chizzen Brain
Mixed and mastered by Chizzen Brain
Stream Ndugu wa mbali E.P now
https://dizastavina.com/ndugu-wa-mbali/
Isingekua hii kitu, zamani ningekua nimebugi.
Rika zangu wengi, mitaani mapanya rodi.
Njamba zimedanja, kisa mkwanja na makugi.
Shamba na mabugizi, mpaka wanabugi.
Nilipotoka mbali aisee, sitaki kurudi.
Huku napiga shugli, medata nimekua ngugi.
Na nikizidaka, nalipa uwanja na kodi.
Nina mama nina bibi, na watoto wanangoja fudi.
Niliamua kuji mix, ruti ndefu niki hiji.
Na sina budi, nikikosa mjini nirudi kijiji.
Msafiri askari wa miguu, kama scobi.
Sai natema madini, ungedhani shimo la mgodi.
Asante kwa Sir godi, simu inaita siku hizi.
Zamani simu inaita kwa mama, mwanae mwizi.
Wala sio ukweli, sema tunaishi na hawa machizi.
Katiza mitaa ya kati, maeneo kama potrizi.
Na mimi pia nina ndoto, inanikosesha hadi usingizi.
Na pia kupata maokoto, kwa tambo kama hizi.
Dunia ina mambo, ya leo sio kama juzi.
Kuishi ni maujanja, na huu upuzi ndio kazi.
Nashukuru kwa pumzi, na improve keep jogging.
Maisha ni kama race, nakua champe Kipchonge.
Kaa kaa kiree, ukiona kiwingu washajilodi.
Kimbia ukiona defender, halafu mjuba umeshasizi.
....
Chorus/Hook scratch..
Nategemewa nyumbani niko mbio.
Kwa hii marathon, mi ni Kipchonge.
Aah aah , Keep jogging.
Marathon mi ni, Kipchonge.
Ah aah long marathon so, Keep jogging.
.....
Verse 2
Mtaani jelasi, walimkwala kwa mama Ima.
Waliondoka na njunja, simu na mpunga wakitaja jina.
Vijana wako kasi, wanangata jiji zima.
Hii ni kama mwendo kasi, inavyopita mzizima.
Hawatoi pasi, hata kandarasi mama pima.
Wako radhi waeke maji, hata kwa nyaya za stima.
Nilianza kujituma, nikajua bloody nikajua kuma.
Nikajua wana, nikajua watu na roho za kutia huruma.
Watakuchekea usoni, ila moyoni wanakusonya.
Wanakuongezea maradhi, kwa story za kukuponya.
Sio marafiki, watakufixi tu ka matonya.
Nishajiuliza nikiwa na dhiki, wangapi watakuja niona.
Au utaniwekea wivu, kipindi navuma.
Au utaeka nguvu, kunishika ili nisirudi nyuma.
Utanitangazia kwa ndugu, siku hizi nakula nguna.
Au ndio mkishakula njugu, muanze kutushikia mazuna.
Tunawaeka juu, hivi mnajua tunachopitia.
Maisha ya ukweli, mpaka wanachukulia uhuni tunausifia.
Tukinyuka pamba, hua ni njaa tunawafichia.
Mi ni hasla kama wewe, siko hivyo unavyofikiria.
Sote ni wahangaikaji, hakuna cha usamaria.
Nishawai kusaidia mskaji, na akarudi kuniibia.
Nilichagua kipaji, na huu mziki ndio nawaimbia.
Na ukiniona niko mbio, kuna mchongo naufukuzia.
.......
Chorus/Hook scratch..
Nategemewa nyumbani niko mbio.
Kwa hii marathon,mi ni kip Kipchonge.
Aah aah Long marathon so, Keep jogging.
.....
Verse 3.
Watu wangu walienda mbali, kuniita Octo ishirini.
Ka Mekatilili, mbio za mashujaa zianze kusini.
Sipati picha ingekuaje, kama singeanza kubuni.
Waliozamia meli, wamekufa afrika kusini.
Tunakwepa kunguni, na vijicho vya mbuni.
Na marafiki wa kweli, hua tunaona kwenye mboni.
Kuna muda hawatusomi, tuko busy vitabuni.
Tunaongeza busara, na hekima ka sulemani.
Nategemewa nyumbani, niko mbioni nazisaka.
Ukifika salasini, na huna hela utadata..
Kuna vitu ukubwani, nimeacha.
Kama kupenda anasa nitachacha, siku hizi nawaza future.
Amani yangu ni muhimu, na hasira hazijengi.
Niliamua kwenda mwenyewe, ilipokua vitu haviendi.
Kama siko show, niko na familia weekendi.
Wakinipenda wao inatosha, hata kama hamnipendi.
Naandika hadithi, haiwezi expire kama status.
Mziki wangu umeshachezwa, mpaka ndani ya state house.
Say my name nikiwa alive, hata nikifa pia.
Nitaacha pengo na nina hakika, nitaacha na historia.
Nilieka Mombasa kwa map, kama atlas.
Sai wananipatia heshima, at last .
Sema ilikua ngumu sana, at first .
Sai tunaisherekea sanaa, art first