POLISI WAUNGA MKONO SHERIA MPYA YA BARABARA ZANZIBAR, HAYA NDIO WANAYOTARAJIA
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
POLISI WAUNGA MKONO SHERIA MPYA YA BARABARA ZANZIBAR, HAYA NDIO WANAYOTARAJIA
3 369 просмотров · 3 дня назад
ASAM Online TV
21,3 тыс. подписчиков
3 369 просмотров · 3 дня назад
Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROAD) umeandaa kikao maalum cha wadau kwa lengo la kupitia na kujadili Rasimu ya Sheria ya Usimamizi na Ulinzi wa Barabara Zanzibar, hatua inayolenga kuimarisha usimamizi, udhibiti na ulinzi wa miundombinu ya barabara nchini.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Barabara, Ndg. Yasser De Costa, amesema sheria iliyopo kwa sasa ni ya zamani na hivyo kuna haja ya kuwa na sheria mpya itakayokwenda sambamba na hali na mahitaji ya sasa.
Amesema rasimu hiyo inalenga, miongoni mwa mambo mengine, kuipa ZANROAD mamlaka zaidi katika kusimamia na kudhibiti shughuli mbalimbali zinazohusiana na barabara, pamoja na kusimamia ujenzi wa miundombinu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Zanzibar, ACP Haji Mkali Haji, amesema Jeshi la Polisi linaunga mkono juhudi hizo, akieleza kuwa iwapo rasimu hiyo itapitishwa na kuwa sheria, itasaidia kuimarisha usimamizi wa barabara na kuchangia katika kupunguza makosa ya usalama barabarani.
Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha rasimu hiyo kabla ya kufikishwa katika hatua za kuipitisha kuwa sheria.
#AsamOnlineTV #Zanzibar #ZANROAD #BarabaraZanzibar #Sheria #UsalamaBarabarani #ZanzibarNews #HabariZanzibar #Miundombinu #TrafficSafety #RoadSafety #Tanzania #ZanzibarUpdates #TikTokTanzania #InstagramTanzania #Trending #FYP #ForYou #Viral #NewsUpdate