DC KARATU: SIKUTOA AGIZO LA KUFYEKA MAZAO/ AKANUSHA TAARIFA ZA MITANDAONI
ITV Tanzania
0:00 / 0:00
DC KARATU: SIKUTOA AGIZO LA KUFYEKA MAZAO/ AKANUSHA TAARIFA ZA MITANDAONI
2 916 просмотров · 1 мес. назад
ITV Tanzania
1,38 млн подписчиков
2 916 просмотров · 1 мес. назад
DC KARATU: SIKUTOA AGIZO LA KUFYEKA MAZAO
#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dkt. Lameck Karanga, amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kwamba aliamuru kufyekwa kwa migomba na miwa ya wananchi wa Kijiji cha Oldeani, Kata ya Endabash, akisema ofisi yake haikutoa agizo hilo.
Dkt. Karanga amesema mgogoro wa eneo hilo umeanza tangu mwaka 2017, kabla hajawa Mkuu wa Wilaya, na kwamba wananchi hao wamekuwa wakielekezwa mara kadhaa kuondoka katika eneo linalodaiwa kuwa la mwekezaji Kongoni Estate.
Amesema mamlaka mbalimbali, ikiwemo uongozi wa wilaya na wataalamu wa kilimo, ziliwahi kuwafikia wananchi hao na kuwaomba kuondoka, akieleza pia kuwa eneo hilo linahusisha vyanzo vya maji.
Kwa mujibu wa Dkt. Karanga, mwekezaji baadaye alifikisha suala hilo mahakamani na wananchi kupewa notisi za kuondoka kupitia court broker. Hata hivyo, amesema yeye alikutana na pande zote na kuwataka wananchi wapewe muda wa kuondoka kwa amani.
“Yaliyotokea siyo maagizo ya Mkuu wa Wilaya. Mimi kwanza nimeona kwenye social media. Mimi sikuagiza watu kwenda pale,” amesema.
Aidha, Dkt. Karanga amekanusha madai kwamba wananchi hao walipigwa viboko kwa maagizo yake, akisema ofisi yake wala Jeshi la Polisi hawakuhusika na tukio hilo.
Ametoa wito kwa wananchi kutovamia maeneo ya watu wala kujichukulia sheria mkononi, huku akiwataka waandishi wa habari kusikiliza pande zote kabla ya kuripoti kuhusu migogoro ya aina hiyo.