SMZ KUJENGA KITUO KIPYA CHA MABASI NA DALADALA BWAWA LA MWANAKWEREKWE
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
SMZ KUJENGA KITUO KIPYA CHA MABASI NA DALADALA BWAWA LA MWANAKWEREKWE
3 438 просмотров · 2 дня назад
ASAM Online TV
22,1 тыс. подписчиков
3 438 просмотров · 2 дня назад
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kujenga kituo kipya cha mabasi na daladala katika eneo la Bwawa la Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa, wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe katika Baraza la Wawakilishi, Chukwani.
Amesema kwa upande wa magari ya wananchi, Serikali imejenga eneo maalum la maegesho katika Soko la Mwanakwerekwe, lenye uwezo wa kuchukua magari takribani 150 kwa wakati mmoja.
Aidha, Mhe. Kitwana amesema Serikali imefanya mazungumzo na ZSSF kuhusu ujenzi wa kituo cha daladala katika eneo la Jumbi, ambapo ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Hatua hizo zinalenga kuboresha huduma za usafiri na maegesho pamoja na kupunguza changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo hayo.
#AsamOnlineTV #Zanzibar #Mwanakwerekwe #Jumbi #Daladala #Usafiri #Maegesho #SMZ #SisiNiJamii